MALI-SIASA-ULINZI

Ufaransa yasitisha operesheni za pamoja za kijeshi na vikosi vya Mali

Wanajeshi wa Ufaransa kutoka operesheni Barkhane wakipiga doria nchini Mali (picha ya kumbukumbu)
Wanajeshi wa Ufaransa kutoka operesheni Barkhane wakipiga doria nchini Mali (picha ya kumbukumbu) Reuters/Benoit Tessier

Ufaransa imesimamisha kwa muda operesheni za pamoja za kijeshi na vikosi vya Mali, kulinana na duru za kuaminika kutoka wizara ya jeshi ya Ufarans, na kubainisha kuwa uamuzi huu unahusiana na mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea nchini Mali na kwamba utahakikiwa tena katika siku zijazo.

Matangazo ya kibiashara

"Mahitaji na mstaru mwekundu vimewekwa" na Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Afrika "kufafanua mfumo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Mali," wizara hiyo imesema. "Ni juu ya mamlaka ya Mali kujibu haraka."

"Kwa kusubiri jibu kutoka kwa mamlaka ya Mali, Ufaransa (...) imeamua kusitisha, kama hatua ya tahadhari na ya muda mfupi, operesheni za kijeshi za pamoja na vikosi vya Mali pamoja na ujumbe wa kitaifa wa ushauri kwa manufaa yao", imeongeza Wizara hiyo. "Tutaondoa maafisa wetu wote wa mipango na programu katika wafanyakazi wa jeshi la Mali pamoja na maafisa wetu wa uhusiano katika jeshi na DGSE," kimeongezea chanzo cha juu cha jeshi la Ufaransa.

Kwa hivyo Paris inasubiri majibu kutoka kwa mamlaka ya Mali kwa madai yaliyowekwa katika siku za hivi karibuni na ECOWS na Umoja wa Afrika. AU Jumatatu ilitaka jeshi la Mali "kurudi haraka na bila masharti katika kambi zake" na kuweka masharti ya kurudi kwa nchi hiyo katika mfumo wa kidemokrasia "bila kizuizi, uwazi na haraka". ECOWAS, kwa upande wake, ilitaka kuteuliwa mara moja kwa waziri mkuu kutoka mashirikaya kiraia.

Wizara ya Vikosi vya jeshi vya Ufaransa imebainisha kuwa "maamuzi haya yatahakikiwa tena katika siku zijazo kulingana na majibu ambayo yatatolewa na mamlaka ya Mali".