SUDAN-USALAMA

Makabiliano ya kikabila yaua thelathini na sita Darfur

Wakimlbizi wa ndani waliokimbilia katika kambi ya ZamZam IDP huko Al Fasher, kaskazini mwa Darfur Aprili 13, 2010.
Wakimlbizi wa ndani waliokimbilia katika kambi ya ZamZam IDP huko Al Fasher, kaskazini mwa Darfur Aprili 13, 2010. REUTERS - Zohra Bensemra

Watu 36 wameuwa Kusini mwa jimbo la Darfur nchini Sudan, baada ya mapigano kuzuka kati ya kabila la kiarabu na lile lisilo la kiarabu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Mashuhuda wanasema, mapigano hayo yalizuka Jumamosi iliyopita, kati ya kabila la kiarabu la Al-Taisha na lile la watu weuzi Fallata, katika eneo la Um Dafuq, Kusini mwa jimbo la Darfur Kusini.

Shirika la Habari nchini Sudan, SUNA, limeripoti kuwa baada ya kuzuka kwa mapigano hayo, jeshi lilitumwa kutuliza makabiliano hayo yaliyowaacha watu wengine 22 na majeruhi.

Haijafahamika chanzo cha mapigano hayo lakini, mara kwa mara mapigano ambayo yamekuwa yakishuhidiwa ni kwa sababu ya mzozo wa ardhi na maji.

Mwezi Aprili, watu wengine 132 waliuawa Magharibi mwa jimbo hilo baada ya mapigano ya kikabila na kuilazimu serikali kutangaza hali ya hatari katika eneo hilo.

Tangu mwaka 2003 jimbo la Darfur limeendelea kushuhudia utovu wa usalama na mwisho wa mwezi Desemba mwaka uliopita, jeshi la Umoja wa Afrika na lile la Umoja wa Mataifa lilimaliza operesheni zake katika jimbo hilo.