MALI-SIASA

Mali: Kanali Assimi Goïta aapishwa rasmi kuwa rais mpya wa mpito

Wafuasi wa Kanali Assimi Goïta, Juni 7 huko Bamako, wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi huyo.
Wafuasi wa Kanali Assimi Goïta, Juni 7 huko Bamako, wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi huyo. AFP - ANNIE RISEMBERG

Kanali Assimi Goïta ametawazwa kuwa rais wa mpito katika mji mkuu wa Mali, Bamako Jumatatu hii, Juni 7. Amehakikisha kuwa Mali "itaheshimu ahadi zake".

Matangazo ya kibiashara

Ameelezea nia yake kuandaa uchaguzi wa haki kwa wakati muafaka, huku akiongeza kuwa "Mali itaheshimu ahadi zake".

Katika hotuba yake pia ametanaza kupunguzwa kwa kiwango cha maisha cha serikali akibaini: "Theluthi mbili ya fedha za zinazotumiwa na ofisi ya rais zitafutwa", ni kusema faranga za CFA Bilioni 1.8 kwa mwaka, ambazo kwa sasa "zitatumika kusambaza maji na kujenga vituo vya afya kwa wenye hali duni katika nchi nzima”.

Rais wa mpito amesema anataka kubadilisha mambo. Katika eneo ambako kulifanyika sherehe hiyo, Choguel Maïga, anayeshukiwa atateuliwa kwenye wadhifa wa waziri mkuu, ameonekana akikaa mbele kana kwamba uteuzi wake ulikuwa ni suala tu la wakati.