DRC-USALAMA

Hospitali moja yateketezwa Boga, Mashariki mwa DRC

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS

Hospitali imeteketezwa moto katika mkoa wa Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika eneo ambalo mapigano yameendelea kushuhudiwa kati ya serikali na makundi ya waasi kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya hali ya dharura kutangazwa katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Shirika ma Madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, wamethibitisha kuteketezwa kwa hospital hiyo katika eneo la Boga, Kusini mwa jimbo la Ituri, siku ya Jumatatu.

MSF inasema, kabla ya kuteketezwa moto kwa hospital hiyo, duka la dawa na bohari la kuhifadhia dawa hizo ilivunjwa, kabla ya hospital hiyo kutekezwa moto.

Watoto tisa waliokuwa katika wodi ya watoto na wagonjwa wawili wamelazimika kupelekewa katika hospital nyingine, baada ya tukio hilo MSF inasema haina taarifa ya watu waliotekeleza kitendo hicho, lakini jeshi la DRC linawashtumu waasi wa ADF.

Hili limejiri wakati huu jeshi likiendeleza operesheni katika maeneo ya Boga, Tchabi karibu na mpaka wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Tarehe 31 mwezi Mei watu karibu 50, waliuawa baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha katika vijini viwili vya Boga na Tchabi.