COTE D'IVOIRE-USALAMA

Mwanajeshi wa Côte d'Ivoire auawa kaskazini mwa nchi

Wanajeshi wa Côte d'Ivoire, huko Buake.
Wanajeshi wa Côte d'Ivoire, huko Buake. Photo: Issouf Sanogo/AFP

Mwanajeshi wa Côte d'Ivoire aliuawa Jumatatu jioni katika shambulio katika mji wa Tougbo, karibu na mpaka na Burkina Faso, kulingana na chanzo cha kijeshi Jumanne hii.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya serikali vilizima haraka shambulio hilo na washambuliaji wakarudi nyuma, Lassina Doumbia, mkuu wa jeshi la Côte d'Ivoire, amesema katika taarifa, na kuongeza kuwa hakuna majeruhi yaliyotokea upande wa raia.

Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo lakini mkoa huo tayari umekuwa ukilengwa na mashambulio ya makundi ya kijihadi yanayoendesha harakati zao katika eneo  hilo.

Makundi yenye mafungamano na Al Qaeda na Islamic State yako katika nchi zinazopakana na Côte d'Ivoire na hufanya mashambulizi kuelekea Kusini.