DRC

DRC: Jino la Patrice Lumumba kurudishiwa familia yake Juni 21

Patrice Lumumba katika nyumba ya Anicet Kashamura, huko Léopoldville, Oktoba 9, 1960.
Patrice Lumumba katika nyumba ya Anicet Kashamura, huko Léopoldville, Oktoba 9, 1960. © AP/H. Babout

Tarehe hiyo sasa imethibitishwa, jino la Patrice Lumumba mtetezi huyu wa Uhuru wa DRC na mpambanaji dhidi ya ukoloni aliuawa mwezi Januari 1961 kabla ya mwili wake kumwagiwa tindikali.

Matangazo ya kibiashara

Jino hili la Patrice Lumumba lilipatikana miaka mitano iliyopita kwa binti ya afisa wa polisi wa Ubelgiji aliyehusika wakati huo na kutoweka kwa mwili wa shujaa huyo. Zoezi hili litafanyika Juni 21, kabla ya mabaki ya waziri mkuu wa zamani wa DRC kuanza safari kwenda DRC hadi Juni 30.

"Kutakuwa na makabidhiano kwa familia na mara tu, mahali hapo, Ikulu ya Egmont [huko Brussels], kutakuwa na makabidhiano rasmi na mamlaka ya Ubelgiji na mamlaka ya DRC. Rais Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo atakuwepo kwa sherehe hii ”, amesema Balfu Bakupa Kanyinda, mtengenezaji wa filamu kutoka Ubelgiji mwenye asili ya Congo, aliyepewa jukumu na mamlaka ya DRC kuratibu sherehe hizi.

"Mnamo Juni 23, mabaki ya Patrice Lumumba yatawasili kwenye ardhi yake ya asili huko Onalua ambapo alizaliwa. Onalua ilipewa jina la "Lumumba-ville" miaka miwili iliyopita na huko, kutakuwa na maombolezo ya ukoo, maombolezo ya familia yake. Asubuhi ya tarehe 25, mwili wa Patrice Lumumba utasafirishwa katika ngome yake ya kisiasa, mjini Kisangani, na tarehe 26, utafikishwa Lubumbashi, alipouawa. Tarehe 27, mwili wa shujaa huyo utasafirishwa mjini Kinshasa ambapo, wakazi wa mji huo watatoa heshima zaokwa kiongozi huyo. Na Juni 30, atazikwa mahali paitwapo Échangeur de Limete, ”amesema Balfu Bakupa Kanyinda.

Mfalme Philippe wa Ubelgiji hatasafiri kwenda Kinshasa Juni 30 kwa mazishi ya kitaifa ya Patrice Lumumba kwa sababu ya mgogoro wa kiafya.