AFRIKA

EU kusaidia baadhi ya nchi za Afrika kukabiliana na baa la njaa

Umoja wa Mataifa unasema watu Milioni 12.8 wanakabiliwa na baa la njaa katika nchi za Afrika Mashariki kama Ethiopia, Somalia, Sudan, South Sudan, Kenya, na Uganda.
Umoja wa Mataifa unasema watu Milioni 12.8 wanakabiliwa na baa la njaa katika nchi za Afrika Mashariki kama Ethiopia, Somalia, Sudan, South Sudan, Kenya, na Uganda. AP - Jerome Delay

Umoja wa Ulaya umesema utatoa Euro Millioni 50 kwa mataifa ya eneo la Sahel na Afrika Mashariki, ili kukabiliana na baa la njaa.

Matangazo ya kibiashara

Hilo limebainishwa na rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, wakati akiwahotubia wabunge wa bunge la Umoja wa Ulaya waliokutana mjini Strasbourg, Mashariki mwa Ufaransa.

Tunahitaji kuimarisha mfumo wa dunia wa upatikanaji wa chakula, ndio sababu Umoja wa Ulaya na G7 tutatoa Euro Milioni 250 kusaidia upatikanaji wa chakula na kukabiliana na baa la njaa, na mfano ni kuwa tutatoa msaada wa Euro Milioni 50 kwa mataifa ya  ukanda wa Sahel na Afrika Mashariki, amesema rais wa tume ya Umoja wa Ulaya.

Umoja wa Mataifa unasema watu Milioni 12.8 wanakabiliwa na baa la njaa katika nchi za Afrika Mashariki kama Ethiopia, Somalia, Sudan, South Sudan, Kenya, na Uganda.