UFARANSA-SAHEL

Macron kuelekea kutangaza kupunguza idadi ya askari wa Barkhane Sahel

Paris imepeleka wanajeshi wapatao 5,100 dhidi ya wanajihadi wenye mafungamano na kundi la Islamic State (IS) na al-Qaeda, msaada mkubwa kwa majeshi dhaifu ya nchi za Sahel ambao wameshindwa kukabilina na wanamgambo hao.
Paris imepeleka wanajeshi wapatao 5,100 dhidi ya wanajihadi wenye mafungamano na kundi la Islamic State (IS) na al-Qaeda, msaada mkubwa kwa majeshi dhaifu ya nchi za Sahel ambao wameshindwa kukabilina na wanamgambo hao. © AFP/Dominique Faget

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anajiandaa kutangaza kuanza kwa zoezi la kuondoka kwa wanajeshi wa kikosi cha operesheni ya kupambana dhidi ya makundi ya kijihadi (Barkhane), hasa nchini Mali, eneo kulikoripotiwa hivi karibuni mapinduzi mapya,shirika la habari la AFP, limesema likinukuu vyanzo vitatu vilivyo karibu na faili hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii, ambayo maelezo yake bado hayajajulikana, ni sehemu ya kisiasa ambayo tayari imeainishwa na rais wa Ufaransa kupunguza uwepo wa wanajeshi la Ufaransa katika eneo hilo kwa muda mfupi.

Emmanuel Macron alikuwa anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari juu ya maswala ya kimataifa leo alasiri. Mkutano huo ambao hapo awali ulipangwa saa 10:30 jioni, ulitarajiwa kucheleweshwa hadi saa 11:00 jioni (sawa na saa 9:00 alaasiri saa za kimataifa).

Yakihojiwa na AFP, makao makuu ya jeshi yamekataa kujieleza kuhusu hatima ya jeshi la Ufaransa, bada ya kufanya kazi katika ukanda huo kwa miaka nane.

"Ni wazi Ufaransa haikusudii kubaki milele katika ukanda wa Sahel. Inawezekana kwamba kikosi cha Barkhane kitalazimika kubadilishwa", meitangaza kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, ambaye yuko ziarani mjini Abidjan.

Paris imepeleka wanajeshi wapatao 5,100 dhidi ya wanajihadi wenye mafungamano na kundi la Islamic State (IS) na al-Qaeda, msaada mkubwa kwa majeshi dhaifu ya nchi za Sahel ambao wameshindwa kukabilina na wanamgambo hao.