ETHIIOPIA-USALAMA

UN: Watu wapatao 350,000 wanakabiliwa na njaa katika eneo la Tigray

Wakimbizi wa nadani wakipewa chakula katika kambi ya mji wa Adigrat, katika jimbo la Tigray.
Wakimbizi wa nadani wakipewa chakula katika kambi ya mji wa Adigrat, katika jimbo la Tigray. © RFI/ Sébastien Németh

Tathmini ambayo haijachapishwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutoa misaada inabaini kamba watu wapatao 350,000 wanakabiliwa na njaa katika jimbo la Tigray uliokumbwa na mizozo nchini Ethiopia, kulingana na hati ya ndani ya Umoja wa Mataifa ambayo shirika la ahbari la REUTERS limepata kopi.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ethiopia inafutilia mbali tathmini hiyo ya Ujumuishaji  wa Usalama wa Chakula na Lishe -(Intergrated Food Security Phase Classification-IPC), kulingana na maelezo kutoka kwa mkutano uliofanyika Jumatatu na Kamati ya Kudumu ya mashirika ya kutoa huduma (IPC au IASC) - iliyoundwa na wakuu wa mashirika yasiyopungua 18 ya Umoja wa Mataifa na yasiyo kuwa ya umoja huo.

Njaa ilitangazwa mara mbili katika muongo mmoja uliopita -nchini Somalia mwaka 2011 na Sudan Kusini mwaka 2017, kulingana na IPC. Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya kutoa misaada, serikali na mashirika mengine yanayohusika hutumia IPC kufanya kazi pamoja ili kujua hali ya mambo.

"Kuhusu hatari ya njaa, ilibainika kuwa takwimu ambazo hazijachapishwa za tathmini ya IPC zilipingwa na serikali ya Ethiopia, hasa watu 350,000 wanaokadiriwa huko Tigray kuwa wanakabiliwa na njaa kwa kiwango cha IPC 5", imebaii hati hiyo.

Hati hiyo pia inasema kwamba utathmini iligundua kuwa mamilioni zaidi ya watu kkatika jimbo nzima laTigray wanahitaji chakula cha dharura na msaada wa kilimo na pia ili kuepuka kukabiliwa zaidi na njaa.

Mapigano huko Tigray yalizuka mnwezi Novemba kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa chama cha zamani cha mkoa huo, Tigray People's Liberation Front. Wanajeshi kutoka nchi jirani ya Eritrea pia waliingia kati katika mzozo huo kuunga mkono serikali ya Ethiopia.

Machafuko huko Tigray yameua maelfu ya watu na kusababisha mamia ya maelfu kutoroka makazi yao katika eneo hili lenye milima, ambalo lina zaidi ya watu milioni 5.