Rais Felix Tshisekedi aahidi neema kwa waathiriwa wa Volkano atetea hatua ya hali ya dharura

Rais wa DRCongo Félix Tshisekedi  Paris Mai 19 2021.
Rais wa DRCongo Félix Tshisekedi Paris Mai 19 2021. AP - Ludovic Marin

Rais wa Jamhuri ya Kidemkorasia ya Congo, Félix Tshisekedi anazuru mji wa Goma tangu Jumamosi. Jumapili hii, Juni 13, alizungumza kwa mara ya kwanza juu ya sababu za safari yake katika jiji hilo, ambalo liliathiriwa na mtiririko wa lava kufuatia mlipuko wa volkano wa Mei 22. Kiongozi huyo wa nchi ya Kongo ametoa taarifa kuhusu mahitaji ya kibinadamu, lakini pia usalama katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waandishi wa habari rais wa Kongo amewahakikishia juu ya msaada utakaopewa waathiriwa wa Volcano. Félix Tshisekedi ameahidi kufanya kila linalowezekana ili kuharakisha uanzishaji wa ujenzi wa nyumba za muda kwa zaidi ya watu 15,000 ambao nyumba zao zimeharibiwa, amesema kuwa kuanzia Jumatatu hii, atatembelea maeneo ambayo yametambuliwa katika suala hili.

 

Alithibitisha azma ya serikali yake kuongeza kasi ya mchakato wa kupunguza Ziwa Kivu, ili kuepuka janga kubwa zaidi katika siku zijazo, lakini pia tafakari juu ya uwezekano wa kupanuliwa kwa jiji la Goma ambalo liko karibu kilomita ishirini kutoka hatari volkano ya Nyiragongo. "Lakini swala hilo halitafanyika kwa haraka na hakuna haki ya mtu itayopokonywa," alisema.

Kuhusu hali ya dharura iliotangzwa huko Ituri na Kivu Kaskazini kwa zaidi ya mwezi mmoja,Felix Tshisekedi amesema atakagua maendeleo yaliyopatikana na udhaifu uliobaki kwa sababu, alisisitiza, " swala hili sio la kimazigaombwe". Kwa hivyo atasafiri kwenda Ituri kuangalia hali ya usalama. Mkuu wa nchi ya Kongo atangaza kwamba pia atakwenda Beni. Vurugu katika eneo hilo zinaendelea licha ya hali ya dharura.

Siku tatu kabla ya kuwasili kwa Félix Tshisekedi huko Goma, watu wasiopungua 9 waliuawa na washukiwa wa wapiganaji wa ADF katika kijiji cha Mutuweyi-Mayamoto, mpakani kati ya majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri. Huko Ituri, habari hiyo inaonyeshwa na mashambulio yanayolenga maeneo ya Tchabi na Boga. Katika ripoti yake, Felix Tshisekedi anaonyesha kusikitishwa na mashambulio haya, lakini pia anapongeza hatuwa chanya iliofikiwa na jeshi huku akiahidi kuendeleza shikizo dhidi ya waasi.

"Hali ya dharura imeamuliwa kwa sababu wakati fulani ililazimika kutumia nguvu. Kikosi hiki kitatumika hadi kukabiliana na ngome ya mwisho ya wahalifu. "Baada ya kutathmini hali hiyo, kutakuwa na mabadiliko." Ukweli ni kwamba katika safu ya vikosi vya jeshi la kitaifa kulikuwa na kasoro kadhaa, tayari ninafanya kazi huko na ninakusudia kufanya kazi huko. "

Mkuu wa nchi pia aliahidi kuharakisha mchakato wa DDR kushughulikia wapiganaji wanaondoka katika makundi yenye silaha.

Ushirikiano ulioimarishwa na Uganda

Bado huko Kivu Kaskazini, atasafiri kwenda Kasindi, mpakani na Uganda, haswa kukutana na mwenzake Yoweri Museveni. Itakuwa swali la kufanya maendeleo kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ambayo itaunganisha Goma na eneo la Uganda, haswa kwa lengo la kupigana dhidi ya biashara zinazohusiana na vitendo vya uhalifu.

Tayari imetajwa katika 2019, mradi wa ujenzi wa barabara unaounganisha Uganda na DRC uliongezeka mnamo 2021 na kutiwa saini kwa nchi mbili mikataba miwili. Barabara kuu tatu zina wasiwasi: Kasindi - Beni, urefu wa kilomita 80; Beni - Butembo, umbali wa kilomita 54 na Bunagana - Rutshuru - Goma urefu wa kilomita 89.

Kwa rais wa Kongo, mradi huu lazima utimie kabisa. "Ninaamini, hii pia itachangia katika kutafuta amani na kutokomeza vikundi vyenye silaha, ambao wengine hutumia vurugu kufanya biashara."

Wajumbe wa baraza lake la mawaziri wanasema kwamba Rais wa sasa wa Umoja wa Afrika, Félix Tshisekedi anaamini katika suluhisho za pamoja na za kikanda, kutatua kabisa shida za ukosefu wa usalama mashariki mwa nchi yake. Ni kwa mwelekeo huu kwamba anahimiza ujumuishaji wa nchi yake katika jamii ya Mataifa ya Afrika Mashariki.