Baraza la Kitaifa nchini Libya halina nguvu mbele ya wanamgambo wanaopigana huko Ajaylat

Des membres d'une alliance de milices islamistes à proximité de Ajaylat.
Des membres d'une alliance de milices islamistes à proximité de Ajaylat. AFP - MAHMUD TURKIA

Mikutano kadhaa ya kiwango cha juu cha usalama ilifanyika Jumatatu, Juni 14 huko Tripoli kujaribu kumaliza mapigano ambayo yamekuwa yakitokea tangu Alhamisi huko Ajaylat, mji ulio kilomita 90 magharibi mwa mji mkuu wa Libya.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu wanane, wakiwemo raia. Baraza la Kitaifa, mamlaka ambayo inaongoza vikosi vya jeshi na usalama nchini Libya, ilitaka kusitishwa kwa mapigano mara moja, ikitishia kuingilia kati.

Licha ya onyo kutoka kwa mamlaka huko Tripoli, magari kadhaa ya jeshi ya wanamgambo wa Zawiya walielekea Jumatatu katika mji wa Ajaylat, uliotawaliwa na wanamgambo wengine wa eneo hilo. Hali inabaki kuwa ya wasiwasi sana. Haijulikani ni nini kilisababisha mapigano ambayo yamedumu kwa siku tano. Wanamgambo wa Ajaylat pia walipokea nyongeza ya silaha.

Silaha nzito

Mapigano hayo yameendesha familia kadhaa kutoka jiji la Ajaylat. Wanamgambo walitumia silaha nzito na makombora yakaanguka kwenye soko na kwenye nyumba. Maduka yameporwa na kuteketezwa. Watu wametekwa nyara.

Baraza la kitaifa linakabiliwa tena na ukosefu wake wa nguvu mbele ya nguvu za wanamgambo ambao hushiriki kupigana wakati wowote masilahi yao yanapokuwa hatarini. Wanamgambo na mamluki ni changamoto mbili kubwa zinazomkabili mtendaji huyo wa muda, ambaye aliwaahidi Walibya mwezi Machi, wakati wa kuapishwa kwake, amani, usalama na utulivu.