UCHAGUZI - ETHIOPIA

Ethiopia: uchaguzi wa wabunge kufanyika katika mazingira ya kuongezeka kwa mgogoro huko Tigray

Wanawake wengine wa Ethiopia wanajiandaa kupiga kura katika uchaguzi wa 2010 wa nchi hiyo.
Wanawake wengine wa Ethiopia wanajiandaa kupiga kura katika uchaguzi wa 2010 wa nchi hiyo. ASSOCIATED PRESS - Jerome Delay

Ethiopia, ambayo ni nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, inajiandaa kwa uchaguzi muhimu na ambao tayari haujakamilika mnamo Juni 21, dhidi ya hali ya njaa katika mkoa unaopigana wa Tigray.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Abiy Ahmed ameupa kipaumbele huo ambao takwimu zinaonyesha atashinda uchaguzi huo. Alichukuwa uadhifa  hiyo mwaka 2018 baada ya kuteuliwa na muungano wa chama tawala, mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2019 anatarajia kupata ushindi katika uchaguzi huo. Siku ya Jumatatu, wapiga kura wapatao milioni 37 wataombwa kuchagua wabunge, ambao nao watamteua waziri mkuu.

Baada tu ya uteuzi wake, wakati kukiwa na harakati kubwa ya kupinga serikali, Waziri Mkuu huyo aliwaachilia huru mamia ya wafungwa wa kisiasa, na kutangaza mageuzi makubwa ya kiuchumi uliodhoofika na akafanya uhusiano mzuri na Eritrea, hatuwa ambayo ilipelekea kupeta Tuzo ya Nobel.