USALAMA SOMALIA

Shambulio baya la kujitoa muhanga latokea katika kambi ya jeshi mjini Mogadishu

Maafisa wa usalama wa Somalia wanawasili katika Hospitali ya Madina ambapo waliojeruhiwa kutokana na shambulio la kujitoa muhanga lililolenga kituo cha jeshi huko Mogadishu wanatibiwa Jumanne, Juni 15, 2021.
Maafisa wa usalama wa Somalia wanawasili katika Hospitali ya Madina ambapo waliojeruhiwa kutokana na shambulio la kujitoa muhanga lililolenga kituo cha jeshi huko Mogadishu wanatibiwa Jumanne, Juni 15, 2021. REUTERS - FEISAL OMAR

Kulingana na takwimu za muda kutoka kwa mkuu wa jeshi la Somalia, shambulio la kujitoa muhanga limesababisha mauaji ya watu kumi huku wengine zaidi ya ishirini wakijeruhiwa katika mji mkuu wa Somalia Jumanne (Juni 15). Mtu mmoja alijilipua kati ya vijana walioajiriwa nje ya kambi kubwa ya jeshi jijini hapo. Shambulio hilo bado halijadaiwa na kundi lolote, lakini wapiganaji wakiislam wa Alshabab wanashukiwa.

Matangazo ya kibiashara

Mshambumliaji mmoja wa kujitoa muhanga anadaiwa kuingia katika eneo hilo kama muajiriwa mpya katika jeshi la Somalia. Inasemekana alijichanganya na vijana kadhaa wakisubiri kwenye foleni nje ya kambi ya Jenerali Abdikarim Yusuf Dhagabadan. Ndipo akafungua mkanda wake wa vilipuzi. Lilikuwa shambulio baya zaidi kutokea huko Mogadishu katika miezi 18 baada ya lile lililotokea kwenye kituo cha usalama na kusababisha mauaji ya watu 81.

Shambulio hilo la Jumanne asubuhi limegusa ishara muhimu ikiwa ni moja ya kambi kubwa zaidi za kijeshi nchini, inayopokea waajiriwa na wakufunzi elfu kadhaa. Kambi hiyo  pia imepewa jina baada ya shujaa wa jeshi. Agosti mwaka 2011, Jenerali Dhagabadan aliongoza operesheni kabambe kuuteka mji wa Mogadishu kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Al Shabab waliolazimika kuondoka jijini Mogadishu. Afisa huyo aliuawa  katika shambulio la kigaidi Novemba 2015.

Shambulio hilo pia linakuja wakati jeshi la Somalia linafanya shambulio kubwa la ushindi katika eneo la kusini mashariki mwa nchi, ambalo inasemekana ilisababisha rasmi vifo vya wapiganaji wa kiislam wapatao 200.

Wengine pia wanahusisha hilo na tangazo siku chache zilizopita kwamba wanajeshi wa Marekani walitumwa nchini Kenya. Rais Joe Biden anataka wanajeshi wa ziada kuimarisha vita dhidi ya Al Shabab katika eneo huo. Tangazo lilitolewa kwamba mapema mwaka huu utawala wa Trump ulikuwa umeondoa wanajeshi wote wa Marekani kutoka Somalia.