Waathiriwa wa mlipuko wa Volcano bado wanasubiri kupatiwa suluhu huko kibati

Foleni ya watu waliohamishwa wakisubiri msaada wa chakula Mei 28, 2021 mashariki mwa DRC baada ya mlipuko wa volkano ya Nyiragongo.
Foleni ya watu waliohamishwa wakisubiri msaada wa chakula Mei 28, 2021 mashariki mwa DRC baada ya mlipuko wa volkano ya Nyiragongo. © REUTERS/MEDECINS SANS FRONTIERES

Rais wa DRCongo Félix Tshisekedi atembelea Kibati, mji ulio kwenye umbali wa kilomita ishirini kutoka Goma. Wale waliohamishwa kutokana na  mlipuko wa Volcano ambao bado hawajaweza kurudi nyumbani, wanasubiri kukamilika kwa ujenzii wa kituo cha mapokezi.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya kaya 400 tayari zimehamia kwenye madarasa katika shule iliyo karibu na eneo ambalo litapokea waathiriwa. Watu hawa waliohamishwa kutoka maeneo yaliyo chini ya Nyiragongo.

Haja ya maji safi ya kunywa na chakula

Wanakosa karibu kila kitu. Miongoni mwao ni watoto na wanawake wajawazito. Walifika katika eneo hilo wiki tatu zilizopita. Wanasubiri kwa hamu kupewa huduma ya matibabu, aidha kutoka kwa wafanyikazi wa mashirika ya misaada au kwa serikali. Wakati huu wakiwa hawana maji safi, chakula na makao mazuri zaidi.

Haya ndio matatizo ambayo serikali inataka kutatua, kwa sababu jirani na eneo walipo kwa sasa itajengwa haraka kambi ya mapokezi inayofaa zaidi ambayo itapatikana huduma ya maji safi na dawa ambapo kutakuwa na zahanati zitazokuwa na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza hususan magonjwa ya kupumua na maleria.

Hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa vitanda ishirini na itaweza kufanya upasuaji kuanzia leo mchana. Lakini kando na kifaa hiki cha matibabu, hitaji la haraka ni kukamilisha haraka kituo cha mapokezi kwa waliohamishwa.