Wanajeshi wa Minusma wahofia kuondoka kwa kikosi cha operesheni Barkhane nchini Mali

Askari Mfaransa wa jeshi la Barkhane anashika doria katika mji wa Tin Hama, Mali, mnamo Oktoba 19, 2017.
Askari Mfaransa wa jeshi la Barkhane anashika doria katika mji wa Tin Hama, Mali, mnamo Oktoba 19, 2017. © REUTERS/Benoit Tessier/File Photo

Jukumu la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali lazima linaelekea kuongezwa muda upya mwishoni mwa mwezi, hakuna mabadiliko yanayotarajiwa katika muundo wa operesheni ya vikosi hivyo vya  kulinda amani, lakini tangazo la kumalizika kwa operesheni ya wanajeshi wa Ufaransa Operation Barkhane imeendelea kuzua maswali.

Matangazo ya kibiashara

Minusma haijazungumza lolote kuhusu tangazo hilo la Barkhane, lakini hata hivyo unasema  "unatathmini matokeo yanayoweza kutokea kuhusu kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa, licha ya kutokuficha wasiwasi iliopo.

"Katika maeneo kadhaa, uwepo tu wa Barkhane ni ulinzi tosha," afisa wa jeshi la UN anaelezea, "na tunapopatwa na mashambulio makubwa, wao ndio wanaotutetea. "

Mwezi Aprili, wakati kambi ya Aguelhoc katika mkoa wa Kidal iliposhambuliwa na wanajihadi mia moja, kuingilia kati kwa ndege za Ufaransa ambazo ndizo zilibadilisha muelekeo wa shambulio hilo. Na mifano haikosi, anakumbuka afisa huyu aliyeko Timbuktu na ambaye, bila kudharau taasisi yake, anaelezea kwamba "nguvu, mwitikio, weledi na mshikamano" wa kikosi cha Ufaransa ni rasilimali muhimu ambazo zitakosekana katika tukio la 'dharura.

"Kuondolewa kwa Ufaransa kutaacha uwanja wazi kwa wanajihadi"

Yeye na afisa mwingine wa UN, walioko Mopti, pia walizungumza juu ya kupeana habari, wakihofia kwamba habari ambayo washirika wengine, wa kikanda au wa Umoja wa Ulaya, wangeweza kutoa haiwezikuwa ya kiwango sawa.

Kikosi cha Kifaransa cha Barkhane na walinda amani wa Minusma hawafanyi kazi kwa pamoja: wa kwanza anapambana na ugaidi kupata habari za kijasusi, ana uwezo wa kushambulia wakati Minusma wao kazi yao ni kulinda amani.