wananchi wa Cote d'Ivoire wagawanyika siku mbili kabla ya kurejea kwa Laurent Gbagbo

Maandamano ya waathiriwa huko Abidjan huko Cote d'Ivoire, Jumatatu, Juni 14, 2021, siku mbili kabla ya kurudi kwa Laurent Gbagbo.
Maandamano ya waathiriwa huko Abidjan huko Cote d'Ivoire, Jumatatu, Juni 14, 2021, siku mbili kabla ya kurudi kwa Laurent Gbagbo. © François Mazet/RFI

Wakati zimesalia siku mbili kabla ya kurejea nchini Core d'Ivoire kwa aliekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, wananchi wa taifa ghilo wamegawanyika kuhusu kurejea kwake, baadhi wakipongeza hatuwa hiyo, huku wengine wakiendelea kuomba haki itendeke kutokanana makosa tuhuma zinazomkabili huku wengine wakiona kwamba kipaombele ni maridhiano.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kusafishwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent anatarajia kureja nchini mwake hapo siku ya alhamisi baada ya kusalia nnje ya nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 10.

Hapo jana, kund la watu, wakiwemo vijana na akina mama wamejitokeza kuandamana katika ofisi za Mea wa mji wa Abobo wakidai vyombo vya sheria vimkamate Laurent Gbagbo na kumpeleka korokoroni au kumpa kifungo cha nyumbani kutokana na tuhuma za baada ya uchaguzi zinazo mkabili rais huyo. mmojawapo ni Issiaka Diaby mwenyekiti wa shirika la muungano wa waathirika wa matukio ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2010

"Laurent Gbagbo, kwa jamii fulani za wahasiriwa, ni kama mbwa mwitu ambaye alikuwa akiendeshwa mbali na zizi la kondoo na ambaye yuko mbioni kurudi. Waathiriwa huko Cote d'Ivoire wana kiu ya haki, mmoja kiu cha ukweli, kiu cha toba, kiu cha malipo, kupitia vitendo vya haki ya jinai. Ni kipengee ambacho kila wakati kilikosekana nchini Cote d'Ivoire kuelekea kwenye maridhiano."

Upande wake Mamadou Soromidjo Coulibaly, anaongoza Shirikisho la Kitaifa la Waathiriwa wa Mgogoro huko Cote d'Ivoire (Fémavipelci). haungi mkono mtazamo huo, anakiri kushindwa kwa chaguo la kimahakama na anapendekeza kwa msisitizo maridhiano.

"Kinachotuchanganya ni kwamba watu wanataka maridhiano na haki. Katika nchi hii, tunajua kwamba kila mtu anahusika. Ama tunakwenda kwa upatanisho na tunafuta kila kitu, au tunaenda kwa haki na wote tutachagua mmoja mmoja. Tunachoomba kwao ni kwamba wanauliza msamaha wetu kwa kutukosea. Huwezi kupigania maisha."

 

Mamadou Soromidjo Coulibaly ana wasiwasi hasa kwamba viongozi wa kisiasa "hawana mtazamo huo" Kama mashirika mengine ya waathiriwa, Fémavipelci na CVCI wiki iliyopita walishiriki mapendekezo yao juu ya maridhiano na waziri anayesimamia kesi hiyo, Bertin Konan Kouadio.