Algeria: Chama tawala cha FLN chashinda uchaguzi wa wabunge uliosusiwa kwa kiasi kikubwa

Uchaguzi wa wabunge nchinbi Algeria uliosusiwa na wengi nchini humo
Uchaguzi wa wabunge nchinbi Algeria uliosusiwa na wengi nchini humo AP - Toufik Doudou

Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi nchinbi Algeria (ANIE) imetangaza Jumanne ushindi wa Chama cha Kitaifa cha Ukombozi (FLN) katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika Jumamosi, katika hali ya mzozo wa kisiasa ambapo idadi kubwa ya watu wamesusia. Uchaguzi huo umevunja matumaini ya mabadiliko kwa wale wote waliotarajia.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha Ukombozi cha Kitaifa kimeshinda uchaguzi wa wabunge wa Algeria. Kulingana na matokeo ya muda,chama hicho kimeshinda viti 105 kati ya 407, wagombea huru wamepata viti 78. Chama cha Harakati ya Amani, chama cha Kiisilamu, kinakuja cha tatu na viti 64. Harakati ya Jil Jadid, ambayo inawakilisha vijana na ambayo ilishiriki katika uchaguzi huu, mwishowe ilipata kiti kimoja tu.

Serikali imerekebisha pia idadi ya ushiriki uliotangazwa Jumapili iliyopita, ambayo tayari iko chini kihistoria kwa asilimia 23.03% ya ushiriki, katika historia ya, Algeria haijawahi kupata ufuatiliaji duni kama huo.

Rekodi ambayo haishangazi, hata hivyo, uchaguzi huu wa mapema wa wabunge umesusiwa na sehemu kubwa ya upinzani na pia na wafuasi wa Hirak, wale Waalgeria ambao walikuwa wameonyesha kwa miezi kadhaa ghadhabu dhidi ya Rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika, walilazimishwa kujiuzulu miaka miwili iliyopita baada ya miongo miwili ya utawala, na ambayo inahitaji tangu mwisho wa mfumo na ujio wa mpito wa kidemokrasia.

Kampeni za uchaguzi pia ziliwekwa dosari ya kukamatwa kwa waandishi wa habari au pamoja na viongozi wa harakati za maandamano.

Said Salhi, makamu wa rais wa Ligi ya Algeria ya Ulinzi wa Haki za Binadamu, hafichi uchungu wake na kueleza kwamba Waalgeria wengi walitamani mabadiliko, lakini sasa wanashuhudia matumaini yao yanavyo zikwa.