Waziri mkuu mpya nchini jamhuru ya Afrika ya Kati Henri Marie Dondra akabidhiwa madaraka

Henri Marie Dondra, Waziri Mkuu wa RCA, mnamo 15 Juni 2021 huko Bangui.
Henri Marie Dondra, Waziri Mkuu wa RCA, mnamo 15 Juni 2021 huko Bangui. AFP - BARBARA DEBOUT

Waziri Mkuu mpya, nchini Jamhuru ya Afrika ya kati Henri Marie Dondra amekabidhiwa madaraka hapo jana tarehe 15 Juni huko Bangui katika sherehe zilizofanyika na mtangulizi wake Firmin Ngrebada.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu huyo mpya alikuwa waziri wa fedha tangu 2016, anachukuwa audhifa huo katika nchi ambayo inapitia changamoto za kiuchumi, kisiasa na kiusalama tangu pale waasi walipoanzisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali.

Mbali na hayo Henri Marie Dondra  anatakibarua kigumu cha kuleta mabadiliko na kuwahakikishia wafadhi wa serikali hususan Ufaransa, ambayo hivi karibuni ilitangaza kusimamishwa kwa misaada yake ya kibajeti na kuongoza "mazungumzo ya kitaifa" yaliyotangazwa na Rais wa Jamhuri Faustin Malaika Mkuu Touadéra.

Katika hotuba yake waziri mkuu huyo mpya ameahidi kufua upya mazungumza na kuweka wazi mipango yake ambapo amesema "Tunakabiliwa na maswala ya uhamasishaji wa rasilimali za ndani. Tunapaswa kuanza kubadilisha vyanzo vyetu vya mapato kwa kupanua wigo wa ushuru,

Na chini ya shinikizo kutoka kwa wafadhili ambao wanadai dhamana katika suala la utawala, haki na kuheshimu haki za binadamu kudumisha misaada yao, "mabadiliko haya yataturuhusu kukubaliana ili washirika wetu warudi mezani. Jambo lote ni kujadili na kubadilishana na hiyo ndiyo inafanyika sasa. "

Halafu ujumbe wa "uwazi", "kwa wenzetu wote, ikiwa ni vikundi vyenye silaha ambavyo viko katika mfumo wa APPR, kushiriki katika serikali hii". Na mwishowe "mazungumzo" na "hitaji la kutuliza mazingira ya kisiasa ya nchi yetu".

Tunasubiri sasa kujua muundo wa serikali mpya. Majadiliano yanaendelea na vyama vya kisiasa na mkuu wa nchi. "inahitaji subra kidogo sio kazi rahisi," alisema waziri mkuu huyo mpya.