DRC - SIASA

Chama cha UNC kimewataka wabunge na mawaziri kutoka chama hicho kususia vikao vya bunge

Billy Kambale,katibu mkuu wa UNC, chama cha Vital Kamerhe.
Billy Kambale,katibu mkuu wa UNC, chama cha Vital Kamerhe. © Pascal Mulegwa/RFI

Baada ya hukumu ya kesi ya rufaa ya Vital Kamerhe, mkuu wa zamani wa wafanyikazi katika Ikulu ya Rais Félix Tshisekedi,aliehukumiwa kifungo cha miaka kumi na tatu jela Jumatano Juni 16 kwa ubadhirifu wa zaidi ya Dola milioni 50, zilizokusudiwa ununuzi wa nyumba za kijamii zilizokusudiwa kwa jeshi na polisi, chama chake UNC kinaimani kwamba kiongozi huyo ameundiwa njama za kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha Vital Kamerhe, UNC, kinaimani kuwa kiongozi wake, aliyehukumiwa kwa mara ya kwanza mwaka mmoja uliopita, aliundiwa njama za kisiasa na kinawataka wabunge wa chama hicho walipo katika muungano na rais Tshisekedi, l’Union sacrée de la nation kususia shughuli za bunge.

Mawaziri watano ambao ni wanachama wa chama hicho, wabunge kumi na watendaji wengine katika wadhifa katika taasisi mbalimbali, kama vile Ikulu, walishiriki katika mazungumzo ya kuchukuwa uamuzi huo. Kulingana na watu wa karibu wa chama hicho,  wanasema, kuondoka kwa taasisi bado sio ajenda, licha ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati. UNC inakusudia kuendelea na majadiliano ya ndani ili kupata haki ya kiongozi wake.

Chama hicho kinapanga maandamano kote nchini, maandamano ambayo tayari yako hatarini. Serikali imepiga marufuku mikusanyiko yoyoteya watu zaidi ya 20 kutokana na wimbi la tatu la Covid-19.