DRC USALAMA

DRC: Namna kundi la ADF linavyoendelea kuwa na uwezo wa kutekeleza uhalifu

Kijiji cha Manzalawu (Manzalaho) katika eneo la Beni, Februari 18, 2020, baada ya uvamizi uliosababishwa na waasi wa ADF. takriban watu 15 waliuawa katika kijiji hiki cha wakaazi 1,000 ambao idadi ya watu walikimbia.
Kijiji cha Manzalawu (Manzalaho) katika eneo la Beni, Februari 18, 2020, baada ya uvamizi uliosababishwa na waasi wa ADF. takriban watu 15 waliuawa katika kijiji hiki cha wakaazi 1,000 ambao idadi ya watu walikimbia. © AFP

Wakati Rais Felix Tshisekedi akiendelea na ziara yake mashariki mwa nchi kutathmini matokeo ya hali ya hali ya dharura ya shughuli za jeshi, kundi la wataalam la Umoja wa Mataifa lilichapisha ripoti yake ya mwisho  Juni 16, ambayo kwa sehemu kubwa inazungumzia eneo la Kivu Kaskazini. Hasa, inatoa takwimu za opereheni dhidi  ya shughuli za  ADF, kikundi cha waasi wa Kiislam wenye asili ya Uganda. Kundi la wataalam limewahoji watu zaidi ya 140 kutoka matabaka yote ya maisha.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la wataalam lilibadilisha chati ya shirika la ADF na hali ya juu ya kambi zao na kubainisha kuwa zote zinabaki sawa sawa kama ilivyokuwa kabla ya shughuli za jeshi mnamo 2019. Lakini operesheni hizi zilifankisha kukamatwa kwa washirika kadhaa wa ADF, kulingana na Wataalam wa UN, hali ambayo ilidhohofisha na kupunguza nguvu kazi zao na kuzuia njia zote za kujizatiti

Video na picha za hivi karibuni zinaonyesha kuwa waasi hawa hawana uwezo wa silaha. Hata wanamiliki ndege mbili zisizokuwa na rubani wanazidi kutumia mambu ya kutengenezwa. Takriban wanajeshi 45 na raia 12 walikuwa wahanga kati ya Novemba na Machi. Kulingana na ushuhuda uliokusanywa na kundi la wataalam, chanzo kikuu cha ADF kupata simaha  kinabaki kuwa mashambulizi dhidiya wanajeshi wa FARDC, ambapo inathibitishwa kuwa jeshi hulengwa mara kwa mara na wanaposhambuliwa wakizidiwa nguvu hukimbia na kuacha silaha na ndipo ADF hutumia fursa hiyo.

Utekaji nyara wa raia

Hakuna ushahidi katika ripoti hii kwamba kuna msaada wowote  ADF inaupata kutoka kundi linalojiita Islamic State ISIS, ingawa ADF inadai kuwa ni tawi la ISIS. IIi kuziba nafasi ya wapiganaji waliopoteza maisha katika mapigano na jeshi, kundi hili linaajiri kutoka katika ukanda huo, pamoja na, katika mashambulizi, huwateka raia na kuwaingiza kwa nguvu kwenye kundi hilo na kuwa wapiganaji. Shambulio la gereza la Beni pia lilisemekana kuwa na lengo hili: watu 1,300 kati ya wafungwa 1,455 walitoroka.

Kumbuka kuwa katika maeneo ambayo ADF imeenea, jeshi la Congo FARDC pia linatuhumiwa kwa kutekeleza dhuluma mbalimbali, ikiwemo , ubakaji, mauaji, lakini pia usafirishaji wa kila aina: dhahabu, kakao, lakini pia silaha. Rais Tshisekedi atakuwa Bunia huko Ituri Alhamisi hii, Juni 17.