MALI - USALAMA

Ma kada wa kundi la EIGS wamekamatwa kaskazini mwa Mali

Wanajeshi wa Mali na wanajeshi wa Ufaransa kutoka Operesheni Barkhane wakati wa doria ya pamoja huko Inaloglog, Mali, Oktoba 17, 2017.
Wanajeshi wa Mali na wanajeshi wa Ufaransa kutoka Operesheni Barkhane wakati wa doria ya pamoja huko Inaloglog, Mali, Oktoba 17, 2017. © REUTERS/Benoit Tessier/File Photo

Mapigano yaliripotiwa Nchini Mali, siku ya Jumanne (Juni 15) kati ya wanajeshi wa Niger na Ufaransa, ambao walikuwa wakiongoza operesheni ya pamoja ya upelelezi, dhidi ya wanajihadi kutoka kundi la Jimbo la Kiislamu la Sahara Kuu (EIGS).

Matangazo ya kibiashara

Mwanajeshi mmoja na Niger aliuawa, mwingine alijeruhiwa, na askari wawili wa Ufaransa wa kikosi cha Barkhane pia walijeruhiwa katika operesheni hiyo, kulingana na maelezo yaliyotolewa Jumatano (Juni 16) na wafanyikazi wakuu wa Ufaransa.

Mapigano haya yalifanyika huko Arabane, karibu na Ménaka, nchini Mali, katika eneo la Mipaka mitatu. Eneo ambalo operesheni kadhaa zimefanywa katika siku za hivi karibuni, ambazo zimesababisha kukamatwa kwa viongozi kadhaa wa kundi linalo jiita Islamic State.

Kupelekwa kwa pamoja kwa vikosi vya Barkhane na Niger "bado kunaendelea". Jeshi la Ufaransa linatoa maelezo machache, lakini linaibua magaidi "kadhaa" waliouawa au kukamatwa na kutangaza kukamatwa, Ijumaa iliyopita karibu na Ménaka, ma "kada wa kikundi cha Dola la Kiislam katika Sahara Kuu": Dadi Ould Chaïb, anayejulikana kama Abu Darda au Abu Dardar. Mwanachama wa zamani wa Mujao, kikundi cha jihadi ambacho kilikaa kaskazini mwa Mali mnamo 2012 na Ansar Dine na Aqmi, ambae alijiunga na kundi linalojiita Islamic State. Alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014, alikabidhiwa kwa mamlaka ya Mali na kisha kutolewa Oktoba iliyopita kama sehemu ya mabadilishano ya wafungwa ambayo yalisababisha kuachiliwa kwa mateka wanne, pamoja na Soumaïla Cissé na Sophie Pétronin.

Cha kushangaza ni kwamba mazungumzo haya yalifanywa na Jnim (Kikundi cha Msaada kwa Uislamu na Waislamu), kilichounganishwa na Al-Qaeda, mpinzani mkubwa katika uwanja wa EIGS. Kutoka kwa chanzo cha usalama cha Ufaransa, Abou Darda pia alipitia Al Mourabitoune, kikundi cha wapiganaji kilichoanzishwa na Mokhtar Belmokhtar.

Tangu aachiliwe, Abu Darda amekuwa akitumia haki za jadi katika eneo la Tin Hama, ambapo inaaminika alishiriki katika kuwauwa  watu watatu wanaotuhumiwa kwa wizi mwezi uliopita.

Jeshi la Ufaransa lilisema kwamba wakati wa kukamatwa kwake, Abou Darda alikuwa amebeba "silaha , miwani ya kuona usiku, vazi la kupigana, simu na redio".

Vyanzo kadhaa pia vinaripoti kukamatwa kwa maafisa wengine watatu wa EIGS, pamoja na Rhissa Al Sahraoui, pia nguzo ya zamani ya Mujao, ambaye watafiti kadhaa na wanajeshi wa eneo hilo wanaelezea kama afisa mwandamizi wa kundi la Islamic State, ambae ni mtu wa karibu na mkuu wa shirika hilo katika maeneo hayo, Abou Walid Al Sahraoui.

Jeshi la Ufaransa lilikataa kuthibitisha kukamatwa huku, wala kufafanua ikiwa waliokamatwa walikuwa bado wanahojiwa na jeshi la Barkhane au ikiwa walikuwa tayari wamekabidhiwa kwa mamlaka ya Mali.