DRC - USALAMA

Rais Felix Tshisekedi atupiliambali uwezekano wa mazungumzo na kundi la ADF

 Congo Félix Tshisekedi.
Congo Félix Tshisekedi. Sumy Sadurni / AFP

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Thisekedi anayendelea na ziara yale Mashariki mwa nchi hiyo, amesema hakuna uwezekano wa kujadiliana na kundi la waasi la ADF ambalo limeendelea kutekeleza mauaji ya raia. Leo, kiongozi huyo anatarajiwa mjini Bunia, katika ziara yake ya kuthmini hali ya usalama katika eneo hilo.na Mwandishi wetu Errickson Luhembwe

Matangazo ya kibiashara

Rais wa DRC alipokea wawakilishi wa tabaka mbalimbali za kijamii  ili kupokea maelezo  juu ya mapendekezo yao kufaanikisha mapambano na makundi ya waasi yanayotekeleza mashambulizi yanayolenga raia kwa kiasi kikubwa

Muakilishi wa jamii ya kiislam katika eneo hilo  Cheikh Umudi Bakari amesema:

" kulingana na hali ya uislam , tume mueleza yakuwa yatakiwa aweze kujitetea , namna alivyo fanya mwenzake Joseph Kabila alipokuwa hapa ziharani , kusema kwamba waislam ambao wako Mjini ni raïa , Tuna juwa kuwa Siku za usoni ata weza kuzungumza Mambo kama Haya , kuonesha utofauti kati ya waeilam raïa na walio katika vikundi vya wapiganaji , sababu uislam hauwezi kuruhusu ukatili namna inavyo fanyika hapa katika mji wetu"

Akijibu maswali ya walioshiriki mkutano huo, Rais wa DRC Félix tshisekedi alisema: 

" inapo semwa uzungumze na aduwi ni kama una tambua ubaya , Je hapa aduwi alisema Ana taka Nini sizani ! sasa naji uliza una weza uka jadiliana na anaye kuuwa ? Ina bidi kwanza kumuonyesha kwamba kuna msimamizi , ni anapo sikia kwamba ana banywa ni kwake sasa kuomba mazunguzo pengine kwa njia hiyo ina weza ika eleweka , sababu hatuna kosa nao alafu kwa kipi tunaweza tuka jadiliana nao ! Na muendelezo huu wa mauaji ? Nadhani ina bidi kuwa onyesha kwamba na Sisi tuna uwezo kwa kiwango fulani"

mwaka 2020 zaidi ya raïa 1300 wali uawa kikatili na watuhumiwa waasi wa Uganda ADF mashariki mwa Kongo .