CONGO BRAZZAVILLE- CHINA

China kuisaidia Congo Brazzaville kupata mkopo wa shirika la fedha duniani IMF.

Rais Denis Sassous Nguesso wa Congo Brazzaville na mwenzake wa China XI Jin Ping Julai 05 2016
Rais Denis Sassous Nguesso wa Congo Brazzaville na mwenzake wa China XI Jin Ping Julai 05 2016 © AFP/Ng Han Guan

China imekubali kuangizia upya deni la taifa la Congo Brazaville, waziri wa fedha nchini humo, Rigobert Roger, akisema hatua hiyo itasadia pakubwa, Congo kupata mkopo kutoka shirika la fedha duniani IMF, hatua ambayo imeafikiwa baada ya rais Denis Sassou Nguesso, kufanya mazungumzo na mwenzake wa CHina, Xi Jinping.

Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wa RFI Loicia Martial anasema mazungumzo  kati ya viongozi hawa wawili yalidumu kama nusu saa, nayo yalijikita juu ya namna ya kuboresha ushirikiano kati ya Brazzaville na Beijing.

Miongoni mwa walioshiriki mazungumzo hayo ni pamoja na waziri wa Fedha wa Congo Brazzaville Rigobert Roger Andély na pia msaidizi wa rais wa nchi hiyo, vyombo vya habari vimeripoti.

Marais hao wawili walijadili kwa kina kuhusu swala la deni ambalo ni chanjo cha kuharibika kwa uhusiano wa nchi hiyo na shirika la fedha duniani IMF.

Rais Nguesso ameridhika na matamshi ya mwenyeji wake Xi-Jinping ambaye ameahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha mapendekezo ya nchi yake kuhusu deni linalodaiwa taifa hilo na IMF, na ambalo limedumu kwa muda mrefu.

Mvutano wa IMF na Congo-Brazzaville uliibuka baada ya dunia kushuhudia mlipuko wa janga la Corona, ambapo mataifa mengi yalijikuta katika ugumu wa kuinua chumi na hivyo kushindwa kulipa deni la shirika la fedha duniani IMF

Mwaka wa 2019, China ilikubali kupunguza deni la Congo-Brazzaville kwa kiasi cha faranga za CFA trilioni 1.3 kutoka deni l kiwango cha jumla ya faranga za CFA zaidi ya trilioni 6.