DRC-UCHUMI

Mamlaka ya DRC yafuta leseni za mfanyabiashara Dan Gertler huko Ituri

Mfanyabiashara wa Israeli Dan Getler anayefanya shughuli zake nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
Mfanyabiashara wa Israeli Dan Getler anayefanya shughuli zake nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo © Simon Dawson/Bloomberg via Getty Images

Mfanyabiashara wa Israeli Dan Gertler amejikuta matatani baada ya kunyanganywa leseni ya kuendesha shughuli zake za uchimbaji katika vitalu viwili vya mafuta kwenye jimbo la Ituri. Wizara ya nishati ambayo imetoa taarifa hiyo imefahamisha kuwa vibali hivi vilivyotolewa kwa mfanyabiashara huyo mnamo mwaka 2010 kuruhusu kampuni zake mbili za Caprikat & Foxwhelp kama sehemu ya makubaliano ya uzalishaji, vilikuwa vimemalizika muda wake, ili kuendeleza shughuli mkoani Ituri.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari wizara ya nishati ya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imefahamisha  ni rahisi kulielewa suala hili linalomkabili mfanyabiashara huyu, kwamba vibali vya kuishi pamoja na leseni alizopewa na serikali ya rais Joseph Kabila vimefikia mwisho wa muda uliokubaliwa.

Wizara hiyo pia imeonesha kuwa haitaendelea kushirikiana na Dan Gertler na sasa inataka kukabidhi vitalu hivyo viwili vya mafuta vilivyo chini ya Ziwa Albert kwa mkandarasi mpya.

Hata hivyo mfanyabiashara huyo Dan Getler amekuwa akidai malipo ya malimbikizo yote yaliyotabiriwa chini ya mradi huu.

Miaka kumi baada ya kupata vibali hivi, kambi ya Dan Gertler imeibua kesi hii na kusema haijakubaliana na hatua ya serikali ya Tshisekedi na inadai imepata uthibitisho kwamba Getler amekuwa akishambuliwa kisiasa kwa madai kuwa amejitajirisha na rasilimali za nchi hiyo isivyo halali na kudai kuwa tangu rais Tshisekedi aingie madarakani amekuwa akikabiliwa na shutuma zenye sur aya kisiasa.

Miongoni mwa shutuma hizo ni pamoja na kile anachodai kubadilishwa majina ya kampuni zake mbili Albertine na Woodhaven, ambapo serikali ya Kinshasa ilisema haizitambui.