COTE D'IVOIRE-SIASA

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ataka talaka na mke wake Simone Gbagbo

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na mke wake  Simone Gbagbo Mwaka 2005.
Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na mke wake Simone Gbagbo Mwaka 2005. AFP - KAMBOU SIA

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amewasilisha kesi Mahakamani akitaka talaka dhidi ya mkewe, Simone Ehivet Gbagbo, ambaye wamekuwa pamoja kwa miongo mitatu, hatua ambayo ifanyike ikiwa ni siku nne tuu baada ya Gbagbo kurejea nyumbani nchini Ivory Coast.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika akaunti binafsi ya mtandao wa kijamii wake wakili Claude Mentenon ambaye ndiye wakili wa rais huyo wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ni kuwa Gbagbo alitamani tangu awali kutalikiana na mke wake Bi Simone baada ya mama huyo kukataa kukubali kuachana naye, kwa miaka mingi na tena kwa mara kadhaa.

Laurent Gbagbo, mweye umri wa miaka 76, amekuwa akiishi kwa miaka mingi na mwandishi wa zamani wa habari nchini humo Bi Nady Bamba mwenye umri wa miaka47 hata kabla ya kukamatwa kwake na kupelekwa Hague Uholanzi.

Kiongozi huyo wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, na Bi Simone Ehivet Gbagbo, walishitakiwa katika Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa uhalifu unaohusiana na mzozo uliotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 na 2011, lakini walipatikana bila hatia.

Gbagbo alirejea nchini Ivory Coast tarehe 17 Juni ambako alipokelewa kwa furaha kubwa na nderemo mbele ya wafuasi wa Chama chake cha FPI-GOR.