CAR-UMOJA WA MATAIFA

Antonio Guterres ashutumu matumizi mabaya ya nguvu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres akitoa wito kwa mataifa yote duniani kupinga matumizi ya mabomu ya ardhini
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres akitoa wito kwa mataifa yote duniani kupinga matumizi ya mabomu ya ardhini Michael Sohn POOL/AFP/File

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Antonio Guterres amewasilisha ripoti yake mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa jumatano hii kuhusu hali inayojiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo amebainisha kuwa kumekuwa na maendeleo chanya juu ya hali ya usalama na ya kisiasa katika nchi hiyo, huku akitaka juhudi zaidi kufanyika ili kufikia usalama wa kudumu katika taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake hiyo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amebainisha kuwa amekaribisha maandalizi ya mazungumzo ya amani ambayo yanalenga kuwaleta pamoja wanasheria pamoja na wasimamizi kadhaa wa makundi ya wapiganaji wenye silaha nchi humo.

Hata hivyo Guterres amesema ana wasiwasi mkubwa kuhusu "utumiaji wa nguvu kupita kiasi nchini humo, ambapo kumeshuhudia kuongezeka kwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na unyanyasaji wa kijinsia unaohusishwa na mzozo uliopo nchini.

Ofisi yake katibu mkuu wa umoja wa mataifa pia imebaini visa vya watu kulazimishwa kuhama makazi yao na unyanyapaa zaidi wa makabila na wa kidini.

Guterres ameongeza kuwa Vikundi vyenye silaha vimefanya ukiukaji mwingi wa haki za binadamu na kwamba vimekuwa vikiongeza uhasama dhidi ya kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa Minusca, hali ambayo amesema haikubaliki hasa kuzuiliwa kwa wanajeshi wa Umoja wa mataifa kupiga doria, pamoja na vitisho dhidi ya wafanyikazi wa Umoja wa mataifa, UN.