BURKINAFASO-USALAMA

Askari polisi 11 wa Burkinafaso wameuawa huku wengine wanne haijulikani walipo

Maafisa wajeshi la polisi wa Burkinafaso mnamo 2016 huko Ouagadougou
Maafisa wajeshi la polisi wa Burkinafaso mnamo 2016 huko Ouagadougou © AFP/AHMED OUOBA

Askari polisi 11 wameuawa na wengine wanne haijulikani walipo nchini Burkinafaso wakati wakijielekeza kuchukuwa nafasi ya wenzao waliokuwa kwenye doria kaskazini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na tarifa ya wizara ya Usalama, Shambulio hilo lilitokea Jumatatu Juni 22 majira ya saa tisa mchana wakati washambuliaji walioendesha mtego kati ya tarafa ya Barsalogo na kijiji cha Foubee. Polisi waliouawa walikuwa wanakwenda kushika nafasi ya wenzao waliokuwepo katika eneo hilo kwa ajili ya usalama katika tarafa ya Yirgou.

Kwa mujibu wa mashuhuda walionusurika katika tukio hilo, washambuliaji walizingira magari na ndipo wakatumia silaha aina ya roketi dhidi ya msafara wa magari ya polisi, ambapo kutokana na uwezo wa silaha waliokuwa nao, polisi hao walilazimika kurudi nyuma.

Kwa mujibu wa duru rasmi, Katika shambulio hilo, askari polisi  saba kati ya 22 ndio walionusurika huku wengine wanne hawajulikani walipo, wakati wa shambulio dhidi ya msafara wa magari matano ya polisi. Duru nyinginr zinaeleza kuwa mmoja alipatikana akiwa ameteketea vibaya.

Duru za wizara ya usalama zinaeleza kuwa opereheni za pamoja, polisi na wanajeshi zinaendelea kuwatafuta askari polisi waliotoweka.