COTE D'IVOIRE-SIASA

Waziri Mkuu wa zamani wa Ivory Coast Guillaume Soro ahukumiwa kifungo cha maisha

Waziri Mkuu wa zamani wa Ivory Coast Guillaume Soro, Jijini Paris september 17 2020.
Waziri Mkuu wa zamani wa Ivory Coast Guillaume Soro, Jijini Paris september 17 2020. STEPHANE DE SAKUTIN / AFP

Waziri mkuu huyo wa zamani wa Ivory Coast alipatikana na hatia ya makosa ya uhaini na pia kuhatarisha usalama wake rais wan chi hiyo.Taarifa ya hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Guillaume Soro ilitolewa wakati akiwa hayupo mahakamani, nchini Ivory Coast.

Matangazo ya kibiashara

Wakili wake Affoussiata Bamba Lamine, mkurugenzi wa ofisi yake Soûl tu Soul, pamoja na mbunge wa zamani wa nchi hiyo Ben Souk, kwa upande wao, wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

Miongoni mwa washirika wake wa karibu kama Alain Lobognon, na Rigobert Soro pamoja na Falicieb Sekongo, wao wamehukumiwa kifungo cha miezi 17 gerezani kwa kuvuruga hali ya utulivu wa taifa.

Guillaume Soro ambaye wakati mmoja alikuwa mshirika wa rais Allasane Outtara ,anatuhumiwa kuhusika kwenye njama ya kijeshi ya kufanya mapinduzi mwaka 2019, miezi kadhaa kabla uchaguzi wa urais nchini humo.