AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini kuendelea kuwa chini ya masharti ya kudhibiti kirusi cha Delta

Waafrika Kusini wanasubiri kupokea kipimo cha chanjo ya Pfizer ya COVID-19 Juni 3, 2021, karibu na mji wa Johannesburg. Afrika Kusini inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi barani Afrika na janga hilo.
Waafrika Kusini wanasubiri kupokea kipimo cha chanjo ya Pfizer ya COVID-19 Juni 3, 2021, karibu na mji wa Johannesburg. Afrika Kusini inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi barani Afrika na janga hilo. © AP - Denis Farrell

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza kuwa, kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo vinavyosambaa kwa kasi kutokana na uwepo wa kirusi aina ya Delta, masharti ya kupambana na maambukizi hayo, yataendelea kutekelezwa hadi mwisho wa mwezi Julai.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa masharti hayo ni kuendelea kufungwa kwa shule na maeneo ya kuuza pombe, lakini pia watu hawaruhusiwi kutembea nje kati ya saa tatu usiku mpaka saa 10 Alfajiri.

Wimbi la tatu la Janga la Corona kwa kirusi kipya aina ya Delta linasambaa kwa kasi kubwa ikilinganishwa na virusi vingine kwenye wimbi la kwanza na la pili barani Afrika, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO. 

Takwimu zinaonesha kesi zinaongezeka mara mbili zaidi kila baada ya wiki 6, kirusi hiki kipya cha Delta kinasambaa haraka katika baadhi ya nchi na tayari kimeripotiwa katika nchi 16, kati ya hizo 9 kinasambaa kwa kasi zaidi.