AFRIKA KUSINI-HAKI

Afrika Kusini yaendelea kukumbwa na machafuko, vifo vyaongezeka

Jeshi limejiandaa kutuma maafisa 2,500 kupambana na waandamanaji hao baada ya polisi kuonekana kuzidiwa nguvu.
Jeshi limejiandaa kutuma maafisa 2,500 kupambana na waandamanaji hao baada ya polisi kuonekana kuzidiwa nguvu. REUTERS - SIPHIWE SIBEKO

Visa vya uporaji katika maduka vimeongezeka nchini Afrika Kusini wakati nchi hiyo ikiendelea kukumbwa na vurugu zilizosababishwa na kufungwa jela kwa rais wa zamani Jacob Zuma.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji waligeuza maandamano hayo na kuwa ghasia mwishoni mwa wiki, wakichoma moto, kufunga barabara kuu na kuvamia na kupora maduka.

Watu 45 wamefariki kwenye ghasia zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Jeshi limejiandaa kutuma maafisa 2,500 kupambana na waandamanaji hao baada ya polisi kuonekana kuzidiwa nguvu.

Zuma mwenye umri wa miaka 79 alihukumiwa mwezi uliopita baada ya kukiuka amri ya mahakama ya katiba ya kumtaka kutoa ushahidi mbele ya tume inayochunguza madai ya rushwa wakati wa utawala wake wa miaka 9.