DRC-BURUNDI

DRC na Burundi zatia saini mikataba mbalimbali na kukubaliana baadhi ya mambo

Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, Juni 13, 2020 huko Bujumbura.
Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, Juni 13, 2020 huko Bujumbura. AP - Berthier Mugiraneza

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi na mwenzake wa Burundi Évariste Ndayimishiye, wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiusalama kwa maslahi ya nchi hizo jirani.

Matangazo ya kibiashara

Hili limebainika baada ya mazungumzo ya viongozi hao wawili, jijini Kinshasa, kufuatia ziara ya rais Ndayishimiye nchini DRC siku ya Jumatatu.

Wawili hao walikutana kwa saa mbili kujadiliana kuhusu suala hilo la usalama miongoni mwa mambo mengine muhimu, ikiwemo ujenzi wa reli kati ya nchi hizo mbili.

Rais Evariste Ndayimishiye ameelezea umuhimu wa nchi hizo mbili, kuimarisha mahusiano yao na kushirikiana kwenye masuala ya maslahi ya Burundi na DRC.

Mwezi Oktoba mwaka 2020, jeshi la DRC liliripoti kuwaondoa wapiganaji wa FNL kutoka Burundi katika kambi zao katika mkoa wa Kivu Kusini.

Aidha, Ndayishimiye amesema nchi yake iko tayari kuwapokea raia wa nchi hiyo waliokimbilia nchini DRC.

DRC inapafa hifadhi ya ukimbizi watu zaidi ya 45,000 kutoka Burundi waliokimbia nchi yao kufuatia mgogoro wa kisisa uliibuka mwaka 2O15 baada ya hyati rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu, kulingana na wapinzani wake.