AFRIKA KUSINI-USALAMA

Idadi ya vifo kufuatia vurugu nchini Afrika Kusini yaongezeka hadi 72

Maafisa wa Polisi wanawakamata watu wanaoshukiwa kupora katika jumba la biasharai huko Johannesburg, Afrika Kusini, Jumatatu Julai 12.
Maafisa wa Polisi wanawakamata watu wanaoshukiwa kupora katika jumba la biasharai huko Johannesburg, Afrika Kusini, Jumatatu Julai 12. AP - Yeshiel Panchia

Watu 72 wamepoteza maisha nchini Afrika Kusini kufuatia ghasia zinazoendelea kushuhudiwa kati ya wafuasi wa rais wa zamani Jacob Zuma na maafisa wa usalama.

Matangazo ya kibiashara

Kwa siku tano, wafuasi wa Zuma ambaye amefungwa jela, wamekuwa wakiandamana katika miji mbalimbali, kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wao.

Machafuko hayo yanakwenda sambaba na waandamanaji kufuja mali  katika maduka makubwa nchini humo katika jiji la Johannesburg na mkoa wa KwaZulu-Natal.

Licha ya rais Cyril Ramaphosa kuagiza kutumwa kwa wanajeshi zaidi ya Elfu mbili kuzuia wizi wa mali na maandamano hayo, hali inaoenekana kuendelea kuwa mbaya.

Maafisa wachache wa usalama wameoneakana karibu na maduka yanayoporowa na wananchi wa taifa hilo, huku idadi ya vifo ikiendelea kupanda,hasa kutokana na watu kukanyagana.

Watu wengine zaidi ya Elfu Moja na mia mbili wamekamatwa katika machafuko hayo.

Wafuasi wa Zuma wanasema wataendelea kuandamana hadi kiongozi wao aliyefungwa jela miezi 15 atakapochiliwa huru.