DRC-SIASA

DRC: Jacky Ndala, mshirika wa Moïse Katumbi akamatwa

Wafuasi wa Moïse Katumbi huko Goma Agosti 2018 (picha ya kumbukumbu).
Wafuasi wa Moïse Katumbi huko Goma Agosti 2018 (picha ya kumbukumbu). AFP - ALAIN WANDIMOYI

Nchini DRC bado kunaripotiwa mvutano kati ya chama cha Mosie Katumbi Chapwe, gavana wa zamani wa Katanga na utawala wa rais Felix, kufuatia sheria inayopendekezwa juu ya "uraia wa Congo".

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Mbunge wa kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nsingi Pululu, aliwasilisha kwenye ofisi za Bunge mswada wa sheria ambao unakusudia kutoa nafasi pekee kwa raia wa nchi hiyo waliozaliwa na wazazi wote wazawa, kuwania nafasi kuu za uongozi, mswada ambao hata hivyo umewagawa wananchi wa Congo.

Mchakato huo ulianzishwa na aliyekuwa mgombea urais Noël Tshiani Muadiamvita aliyepata udhamini wa mbunge wa kitaifa Nsingi Pululu kutoka muungano wa zamani wa FCC ambapo amebaini kuwa kinachoendelea nchini humo ni kurejelea tena sheria ya utaifa.

Muswada unawagawa wananchi wa Congo

Nakala hiyo inapingwa vikali na chama cha Moise Katumbi, ambacho, hata hivyo kimetishia kuondoka katika muungano unaotawala. Kwa wale walio karibu na gavana wa zamani wanasema, hatua mpya ilifikiwa Jumapili baada ya kukamatwa kwa Jacky Ndala, mkuu wa vuguvugu la Vijana wa chama cha Moïse Katumbi.

Sababu za kukamatwa kwa Jacky Ndala hazijulikani kwa wale walio karibu naye au kwa chama chake, Ensemble pour la République.

"Amekuwa mwathirika wa vitisho na visa vingine kwa siku tatu zilizopita akiambiwa kuwa atakamatwa na kupelekwa kule wanakotaka kumpeleka. Mwenzetu amedhalilishwa tu mbele ya watoto wake na mkewe, akichukuliwa kama chizi, akitupwa ndani ya gari, "amesema John Padou, msemaji wa vuguvugu la vijana wa chama cha Ensemble pour la République.

Chama cha Moise Katumbi kinanyooshea kidolea cha lawama Idara ya ujasusi kuhusika na kisa hicho cha kumkamata afisa wake, saa chache baada ya makada wengine wa chama hicho kuaachilia na watu wasiojulikana baada ya kukamatwa siku ya Jumamosi.

Chama hicho kinadai kuwa makada hao wawili waliteswa kabla ya kuachiliwa.

Tunajua kwamba Jacky Ndala, kama watu wengi wanaomuunga mkono Katumbi, hivi karibuni amechukua msimamo mkali dhidi ya muswada ambao unaweza kumuweka kando gavana wa zamani wa Katanga kwenye uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwaka 2023.