ETHIOPIA

Mvutano waibuka tena kati ya Ehiopia, Sudan na Misri kuhusu matumlizi ya Nile

Mazungumzo huko Khartoum Desemba 21, 2019 kuhusu matmizi ya Bwawa la Renaissance kwenye Mto Nile (picha ya kumbukumbu).
Mazungumzo huko Khartoum Desemba 21, 2019 kuhusu matmizi ya Bwawa la Renaissance kwenye Mto Nile (picha ya kumbukumbu). AFP Photos/Ashraf Shazly

Joto linapanda kati ya Misri, Sudan na Ethiopia kufuatia hatua ya serikali ya Addis Ababa kujaza bwawa kubwa la kuzalisha umeme  kwa mwaka wa pili kwa kutumia maji ya mto Nile. Khartoum na Cairo, zimeandika barua kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulalamikia hatua hiyo ya Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

Katika kingo za Mto Blue Nile, wafanyikazi karibu 20 wanaendelea na kazi ya kuchanganya tope na mbolea, kutenengeza matofali, yanayoanikwa juani, yanayofahamika kwa jina la TOOB, yanayotumiwa kwenye shughuli za ujenzi katika eneo hilo. 

« Wakati Mto unapojaa, maji yanaziba haya mashimo. Wakati wa msimu wa kiangazi, tunatumia mchango huu kwenye shughuli zetu, kwa hivyo bwawa hili linatuathiri, kwa sababu maji yanapowasili hapa, hayana mchanga tunaohitaji, » amesema Abdallah Adam mmoja wa watu wanaotumia maji ya mto huo kwenye shughuli zao.

Adam anasema hana taarifa zozote kutoka serikalini kuhusu madhara yanayoweza kujitokeza kufuatia ujenzi wa bwawa hilo.

  « Hatuna uhakika. Hatuna taarifa zozote isipokuwa zile tunazoziona kwenye mitandao ya kijamii….Mambo yote yanafanyika kwenye ngazi za kisiasa na sisi watu wa chini hatufahamu chochote…..Kuna maelfu ya watu wanaofanya kazi kwa mikoni yao;…..Mimi sasa nina mashaka, kwa sababu, kingo za mto huu ni tegemeo letu, tunazitegemea kwa uchumi wetu, » amesema Abubakar Issa mmoja wa wavuvi katika mto huo, huku akiongeza madhara yanaanza kujitokeza.

Kwa sasa madhara sio makubwa, lakini kuna mashaka.Ethiopia inapojaza bwawa lake, Sudan nayo inahifadhi maji. Kuna upungufu wa maji.Tunaanza kuona miamba chini ya maji na hii sio dalili nzuri ya kupata samaki, na wakifungua kingo, laji yatakuja kwa kasi na sio nzuri kwa kazi.