MALI-SIASA

Rais wa mpito wa Mali Assimi Goïta aponea kuuawa kwa kisu

Rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta. Hapa, ilikuwa wakati wa sherehe kuapishwa kwake huko Bamako, Juni 7, 2021.
Rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta. Hapa, ilikuwa wakati wa sherehe kuapishwa kwake huko Bamako, Juni 7, 2021. © Annie Risemberg, AFP

Kanali Assimi Goïta ambaye yuko madarakani tangu Mei 24, ameponea kuuawa kwa kisu. Watu wawili wamejaribu Jumanne hii asubuhi kumchoma rais wa mpito wa Mali bila mafanikio, wakati wa ibada ya Waislam ya Eid al-Adha, sikukuu ya kuchinja wanyama walio halali, katika Msikiti Mkuu wa Bamako, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Walipoulizwa na shirika la habari la AFP juu kitendo hicho kama "jaribio la mauaji" ya rais, wasaidizi wake wamejibu: "Ndio, kabisa ni kweli".

"Tunachunguza. Angalau mtu mmoja amejaribu kumshambulia kwa kisu katika Msikiti Mkuu wa Bamako leo," chanzo hicho kimeongeza, kikisema "rais yuko salama na mzima.".

Mapinduzi mawili kwa mwaka mmoja

Akiwa katika eneo la tukio, Waziri wa Masuala ya Kidini, Mamadou Koné, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "mtu amejaribu katika Msikiti Mkuu wa Bamako kumuua rais wa mpito kwa kisu".

Lakini "amedhibitiwa kabla ya kutekeleza uhalifu ho," hanzo hicho kimebaini.

"Ilikuwa baada ya sala na mahubiri ya imamu, wakati imamu alikuwa akijianda kwenda kuchinja kondoo wake, ndipo kijana huyo alijaribu kumchoma Assimi Goïta mgongoni, lakini mtu mwingine ndiye alijeruhiwa," Latus Tourè, msimamizi wa Msikiti Mkuu, amelithibitishia shirika la habari la AFP.

Mali imeshuhudia majaribio mawili ya mapinduzi katika kipindi cha mwaka mmoja. Jaribio la kwanza lilifanyika mwezi wa Agosti 2020 na kisha Mei mwaka huu, majaribio ambayo yaliongozwa na kanali Assimi Goïta, ambaye tangu wakati huo ni rais wa mpito.