UFARANSA

Ufaransa yaanzisha uchunguzi kuhusiana na ujasusi wa Morocco

Miongoni mwa wanahabari ambao wameripotiwa kudukuliwa na mtandao huo wa kijasusi ni pamoja na wale wanaofanya kazi na RFI, Runinga ya France 24, shirika la habari la AFP na Gazeti la Le Monde.
Miongoni mwa wanahabari ambao wameripotiwa kudukuliwa na mtandao huo wa kijasusi ni pamoja na wale wanaofanya kazi na RFI, Runinga ya France 24, shirika la habari la AFP na Gazeti la Le Monde. © Beverly Santu/RFI

Viongozi wa mashtaka jijini Paris nchini Ufaransa, wameanza uchunguzi wa madai ya maafisa wa ujasusi wa Morocco, kutumia kampuni ya masuala ya ujasusi wa mtandao, Malware Pegasus kuwadukua wanahabari wa Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huo unalenga madai 10, ikiwa ni pamoja na iwapo taarifa binafsi za wanahabari hao zilidukuliwa kupitia vifaa vyao vya kieletroniki na mtandao huo wa ujasusi.

Miongoni mwa wanahabari ambao wameripotiwa kudukuliwa na mtandao huo wa kijasusi ni pamoja na wale wanaofanya kazi na RFI, Runinga ya France 24, shirika la habari la AFP na Gazeti la Le Monde.

Uongozi wa France Media Monde umeeleza kugadhabishwa na kuzitaka mamlaka kuchukua hatua dhidi ya wizi wa taarifa.

Hata hivyo, Morocco imekanusha kuhusika na udukuzi huo wakati huu, masharika makubwa ya Habari duniani kama The Washington Post, The Guardian na watu wengine mashuhuri duniani wamekuwa wakidukuliwa na kampuni ya Israel inayofanya shughuli za ujasusi kwa njia ya mtandao NSO.