DRC-HAKI

DRC: Jacky Ndala ahukumiwa kifungo cha miaka 2 jela kutokana na matamshi yake

(Makao makuu ya Bunge, Kinshasa) Bunge lajadili muswada wa sheria ambao unakusudia kutoa nafasi pekee kwa raia wa nchi hiyo waliozaliwa na wazazi wote wazawa, kuwania nafasi kuu za uongozi.
(Makao makuu ya Bunge, Kinshasa) Bunge lajadili muswada wa sheria ambao unakusudia kutoa nafasi pekee kwa raia wa nchi hiyo waliozaliwa na wazazi wote wazawa, kuwania nafasi kuu za uongozi. RFI/Sonia Rolley

Jacky Ndala, kiongozi wa vijana wa chama cha gavana wa zamani Moïse Katumbi amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa matamshi yake dhidi ya muswada unaojulikana ambao unakusudia kutoa nafasi pekee kwa raia wa nchi hiyo waliozaliwa na wazazi wote wazawa, kuwania nafasi kuu za uongozi, mswada ambao hata hivyo umewagawa wananchi wa Congo.

Matangazo ya kibiashara

Muswada huo, ikiwa utapitishwa na kutangazwa, unaweza kuwatenga wagombea kadhaa wa uchaguzi ujao wa urais, akiwemo kiongozi wake Moïse Katumbi, ambao hawakuzaliwa na wazazi wote wawili wenye uraia wa DRC.

Jacky Ndala alikamatwa Jumapili asubuhi na maafisa wa idara ya ujasusi na kufikishwa masaa 24 baadaye kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa jamhuri huko Kinshasa-Matete. Alipofikishwa mbele ya majaji wa mahakama ya Amani ya Kinkole Jumanne, katika vitongoji vya Kinshasa, hatimaye alihukumiwa kifungo ha miaka miwili jela.

Ikiwa Jacky Ndala amefikishwa mahakamani, ni kwa kwa sababu ya matamshi yake alioyatoa kwenye mkutano wake wa mwisho. Alitoa wito wa kuvamia makao makuu ya Bunge ikiwa muswada huo utapitishwa.

Mwezi Julai mwaka jana, mbunge wa kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nsingi Pululu, aliwasilisha kwenye ofisi za Bunge muswada wa sheria ambao unakusudia kutoa nafasi pekee kwa raia wa nchi hiyo waliozaliwa na wazazi wote wazawa, kuwania nafasi kuu za uongozi

Kwa upande wa mwendesha mashtaka, anasema matamshi haya ni kosa "linalochochea utovu wa nidhamu kwa mamlaka ya umma". Hata hivyo mwanasheria wa Jacky Ndala, wakili John Padou, anahoji hoja hii. "Kwetu, chanzo cha waraka huo kinatia shaka. Ibara hiyo inazungumza juu ya raia kupinga sheria, je! Hati ya Pululu ni sheria? Hapana. Ni pendekezo. Je! Ni sheria gani aliyodharau? ... Hukumu hiyo ilitolewa pasikpo kuwa na kosa. Je! Ni marufuku kuandamana hadi makao makuu ya Bunge? Tutatumia njia za kisheria kukata rufaa kwa mujibu wa sheria za DRC ”.