MALI-SIASA

Mali: Masuali yaibuka kuhusu jaribio la mauaji ya Kanali Assimi Goïta

Maafisa wa vikosi vya usalama wanamkamata mmoja wa washukiwa katika jaribio la kumuua Kanali Goïta Julai 20, 2021.
Maafisa wa vikosi vya usalama wanamkamata mmoja wa washukiwa katika jaribio la kumuua Kanali Goïta Julai 20, 2021. AFP - EMMANUEL DAOU

Nchini Mali, rais wa mpito Assimi Goïta alinusurika kifo Jumanne wiki hii katika Msikiti Mkuu wa Bamako Jumanne, Julai 20. Mtu mmoja alimshambulia kwa kisu, lakini mtu huyo hakuweza kufikia malengo yake.

Matangazo ya kibiashara

Kanali Assimi Goïta alinusurika kifo kabla ya vikosi vya usalama kuingilia kati na kuldhibiti mtu huyo, lakini hali hii imeibua maswali mengi nchini Mali. Wengi wametaka kufahamu watu wanaojificha nyuma jaribio hili la mauaji.

Rais wa mpito nchini Mali, baada ya kunusurika jaribio la mauaji kwa kisu, alitoa dalili, juu ya mtu au watu wanaohusika, wafadhili wa kitendo hicho kibaya.

"Unapokuwa kiongozi, kuna watu ambao hawafurahii, watu ambao wakati wowote wanaweza kutaka kujaribu kupitia mambo mbalimbali ili kuzorotesha usalama", amesema Kanali Goïta.

Wachunguzi wanatathmini mazingira ya tukio hilo

"Kuhatarisha usalama", neno limetamkwa, lakini ni nani hasa?

Masaa kadhaa baada ya kukamatwa, mshambuliaji ambaye alionekana amechoka, hakuongea chochote alipokuwa akiulizwa. "Ni wazi alitumia dawa za kulevya kabla ya kuchukua hatua," kilisema chanzo kilio karibu na uchunguzi.

Kuhusu uwezekano wa shambulio la kijihadi, wachunguzi wanaona kuna hitajika vielelezo na ushahidi. Njia nyingine inayowezekana ni uhasama na mvutano katika udhibiti wa madaraka.

Kwa upande wa serikali wanabaini kwamba uchunguzi utabainisha ukweli. Lakini kwa sasa, usalama wa Kanali Assimi Goïta utaimarishwa. Hadi wakati huo alikuwa akisafiri kwa gari ndogo akisindikizwa na pikipiki mmoja tu na msafara wake ulikuwa na magari yasiozidi kumi.