NIGERIA-USALAMA

Watu 100 waokolewa kutoka mikononi mwa kundi la watekaji nyara

Wanafunzi waliookolewa huko Jangebe kutoka kundi la watekaji nyara, Machi 2, 2021, Nigeria.
Wanafunzi waliookolewa huko Jangebe kutoka kundi la watekaji nyara, Machi 2, 2021, Nigeria. REUTERS - AFOLABI SOTUNDE

Wanavijiji 100 waliokuwa wametekwa na watu wenye silaha kwa siku 42 nchini Nigeria, wameachiliwa kwa mujibu wa ripoti za maafisa wa Polisi.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la watu hao (wanawake na watoto) lilitekwa nyara Juni 8 katika jimbo la Zamfara, huku watu wanne pia waliuawa wakati watukio hilo.

Wengi wamekuwa wakiachiliwa huru ikiropotiwa baada ya kulipwa kwa kikombozi, lakini baadhi wamekuwa wakiuawa.

Hata hivyo Serikali ya jimbo la Zamfara imesema kuwa mateka hao waliachiliwa huru bila kikombozi, lakini haikutoa maelezo zaidi.

Serikali inasema watu hao sasa waafanyiwa vipimo vya kimatibabu na kupewa maagizo kabla ya kurejea nyumbani.

Visa vya utekaji nyara vya mara kwa mara vimekuwa vikitokea katika eneo hilo katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.