ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Ishirini waangamia katika mapigano Afar

Waziri Mkuu Abiy Ahmed alituma wanajeshi katika jimbo la Tigray mwezi Novemba mwaka uliopita, kupambana na waasi wa TPLF, makabiliano ambayo yamesababisha mauaji na baa la njaa.
Waziri Mkuu Abiy Ahmed alituma wanajeshi katika jimbo la Tigray mwezi Novemba mwaka uliopita, kupambana na waasi wa TPLF, makabiliano ambayo yamesababisha mauaji na baa la njaa. EDUARDO SOTERAS AFP

Raia 20 wameuwa na maelfu wameyakimbia makwao baada ya kuzuka kwa mapigano makali kati ya waasi na vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya Ethiopia, katika jimbo la Afar linalopakana na lile lenye mzozo la Tigray.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya mapya yanaashiria mwendelezo wa machafuko ya zaidi ya miezi minane katika jimbo la Tigray, eneo ambalo maelfu ya watu wameuawa na wengine kuyakimbia makwao.

Mohammed Hussen, afisa wa idara ya serikali inayohusika na majanga amesema mapigano hayo yameendelea kushuhudiwa siku ya Alhamisi na tayari watu Elfu 70 wameathiriwa moja kwa moja.

Hii inakuja baada ya waasi wa Tigray kulenga vikosi maalum vya jeshi la Ethiopia katika jimbo la Afar, lakini pia walikuwa wanawalenga waasi katika jimbo la Oromia.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed alituma wanajeshi katika jimbo la Tigray mwezi Novemba mwaka uliopita, kupambana na waasi wa TPLF, makabiliano ambayo yamesababisha mauaji na baa la njaa.