CAR-USALAMA

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Mashambulizi mapya yasababisha vifo kadhaa Bossangoa

Karibu na mji wa Bossangoa, Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Karibu na mji wa Bossangoa, Jamhuri ya Afrika ya Kati. © flickr

Kundi la vijana waliuawa Jumatano Julai 21 huko Bongboto, kilomita 12 kutoka Bossangoa. Hakuna idadi rasmi, lakini inaaminika kuwa angalau wat wanane waliangamia katika mashambulizi hayo mapya.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa serikali wanasema, wapiganaji wa muungano wa makundi ya waasi wa CPC ndio walishambulia wanakijiji waliokuwa wakikimbilia karibu na barabara inayo unganisha miji ya Nana na Bakassa. Katika picha inaonekana kuwa waliouawa ni vjana. Uchunguzi umefunguliwa na unaendelea, amesema waziri pia msemaji wa serikali.

Lakini ripoti, kutoka vyanzo viwili vya usalama, zinaonyesha wakati wa tukio hilo, uwepo vikosi vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Afrika ya Kati na vile vile vikosi vya pande mbili vya Urusi. Waziri Djorie, amesema tukio hilo ni mchanganyiko wa mazingira. Vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati, FACA, vilikuwa vikipiga doria kwenye barabara hiyo wakati wa tukio. Baada ya kupata taarifa, walikwenda eneo la shambulio na kusairisha miili katika hospitali ya Bossangoa, amesema.

Tukio hili jipya linatokea katika mkoa huu unaojulikana kuwa ngome ya rais wa zamani na mratibu wa munganowa makundi ya waasi wa CPC, François Bozizé. Uchaguzi mdogo wa wabunge umepangwa kufanyika huko Nana-Bakassa mwishoni mwa wiki hii. Mamlaka imehakikisha kuwa imechukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa usalama.