TUNISiA-USALAMA

Kumi na saba wakufa maji kwenye pwani ya Tunisia

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mamia ya wahamiaji wameangamia katika matukio ya kuzama kwa boti, wakijaribu kuingia Ulaya.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mamia ya wahamiaji wameangamia katika matukio ya kuzama kwa boti, wakijaribu kuingia Ulaya. ANNE CHAON / AFP

Wahamiaji wasiopungua 17 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama, ajali iliyotokea kwenye pwani ya Tunisia, shirika la hilali nyekundu nchini Tunisia limesema.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wahamiaji 380 wameokolewa na maafisa wa kikosi cha walinzi wa pwani ya Tunisia, kulingana na shirika hilo la kibinadamu.

Boti hiyo ilikuwa imetoka pwani ya kaskazini mashariki mwa Libya, ikiwa na wahamiaji kutoka Syria, Misri, Sudan, Eritrea, Mali na Bangladesh.

Matukio kadhaa ya kuzama kwa boti yametokea katika miezi ya hivi karibuni karibu na pwani ya Tunisia, wakati majaribio ya kuvuka Bahari ya Mediterania yanaongezeka kufuatia kuboreka kwa hali ya hewa.

Idadi ya wahamiaji nchini Italia, ambayo ilikuwa imepungua katika miaka ya hivi karibuni, pia imeongezeka tena mwaka 2021.