AFRIKA KUSINI

Pfizer / BioNTech kuzalisha dozi milioni 100 kwa mwaka nchini Afrika Kusini

Kampuni ya Pfizer inasema inataka kuhifadhi chanjo hizi kwa bara la Afrika.
Kampuni ya Pfizer inasema inataka kuhifadhi chanjo hizi kwa bara la Afrika. AP - Stew Milne

Baada ya maabara ya Johnson & Johnson kushirikiana na Aspen, ni zamu ya Pfizer / BioNTech kushirikiana na kampuni ya Afrika Kusini kutoa chanjo yao ya kupambana na janga la Covid.

Matangazo ya kibiashara

Maabara hiyo imesaini makubaliano na Taasisi ya Biovac, kampuni ya serikali yene makao yake makuu huko Cape Town.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa chanjo ya Messenger RNA kutengenezwa barani Afrika. Lengo ni kutoa dozi milioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2023. Uzalishaji unaweza kuanza mapema mwaka ujao. Kampuni ya Pfizer inasema inataka kuhifadhi chanjo hizi kwa bara la Afrika.

Chanjo zinazozalishwa Afrika pekee kwa Waafrika. Huu ndio uhalisi wa toleo la Pfizer. Kwa bara, faida ni kupunguza utegemezi wake kwa nchi za nje. Itakumbukwa kuwa mwezi wa Machi, Taasisi ya Serum kutoka India ilisitisha usafirishaji wa chanjo ya AstraZeneca. India, iliyokumbwa na wimbi kubwa la janga, ilitaka kuhifadhi mahitaji yake ya ndani ili kukabiliana na janga hilo. Walakini, bara la Afrika, kupitia mfumo wa Covax, lilikuwa limeifanya maabara hii kuwa moja ya wauzaji wake wakuu.

Aina hii ya kukatishwa tamaa inapaswa kuepukwa na uzalishaji uliowekwa kwa Waafrika. Kwa upande mwingine, bara la Afrika bado litalazimika kutegemea nje.  Dawa hiyo baada ya kutengenezwa itawekwa katika cmahupa na kusambazwa katika nchi wanachama 55 za Umoja wa Afrika. Hii ni habari njema na nzuri kwa Kituo cha Afrika cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa.