DRC-MAUAJI-WAASI

Raia 16 wauawa karibu na mji wa Beni Mashariki mwa DRC

Uharibifu uliofanywa na waasi wa ADF Mashariki mwa DRC
Uharibifu uliofanywa na waasi wa ADF Mashariki mwa DRC John WESSELS / AFP

Zaidi ya watu 16 wameuawa baada ya kushambuliwa Alhamisi mchana, na watu wenye silaha Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo karibu na mji wa Beni walipokuwa wanatokea sokoni.

Matangazo ya kibiashara

Watu hao walikuwe kwenye Lori waliposhambuliwa katika kijiji cha Kapoka, waliposimishwa na kupigwa risasi miongoni mwao wakiwa wanawake sita, mtoto mmoja na wanaume tisa, huku wanane wakijeruhiwa.

Charles Omeonga mkuu Kiongozi wa wilaya ya Beni anawashtumu waasi wa ADF kwa kuhusika.

Waasi wenye nia mbaya waliwakwepa wanajeshi wetu na kuwashambulia raia, lakini mpaka sasa wamedhibitiwa, wanaendeleza propaganda zao.

Raia wali miminika kunako hospitali teule Mjini OICHA,  kama alivyoleza Daktari  Nzemengo.

Hali ya Oicha ni mbaya, watu wenye silaha waliwauwa watu walikuwa wanatokea sokoni, kuna miili ya watu hapa na wengine wamejeruhiwa, wapo katika hali mahututi.

Usalama unazidi kudidimia licha ya kuwekwa kwa utawala wa kijeshi , Philippe BONANE mmoja wa viongozi wa kirai wilayani Beni  anaeleza hali halisi.

 Tangu kuanza kwa  "état de siège"  hatujaona askari wakipigana na adui

Marekani imelishtumu kundi la ADF kushirikiana na kundi la Islamic State.  

Kwa mujibu wa Kanisa Katoliki nchini DRC, tangu mwaka 2013 raia zaidi ya 6,000 wameuawa na waasi Mashariki mwa  nchi hiyo.