CAR-USALAMA

CAR: Mauaji ya watu 13 Bossangoa yazua mkanganyiko

Wanawake wakifua nguo katika mto wa Ouham, Machi 8 huko Bossangoa.
Wanawake wakifua nguo katika mto wa Ouham, Machi 8 huko Bossangoa. RFI/Charlotte Cosset

Kulingana na vyanzo mbalimnali, waathiriwa, ambao wanaweza kuwa wengi zaidi, walikuwa vijana, wafanyabiashara, ambao walisafiri kwa pikipiki kwenda katika soko la Kouki.

Matangazo ya kibiashara

Serikali mara moja ilishushia lawama muungano wa waasi wa CPC, ambao mkoa huo ni moja wapo ya ngome yake, kuwa ulihusika na mauaji hayo, lakini vyanzo vingi vinashtumu wanajeshi wa Urusi wanaosaidia vikosi vya serikalikatika eneo hilo.

Wakati huo huo muungano wa mavikundi ya waasi wa CPC ambao uliendesha mashambulizi katika mji wa Bangui mapema mwaka ulikanusha kuhusika kwake katika mauaji hayo,kulingana na taarifa ya muungano huo. Umesikitishwa na kuhusishwa na mauaji hayo (...) bila hata hivyo kusubiri matokeo ya uchunguzi wa kawaida". Makundi hayo yenye silaha yamebaini kwamba watu waliouawa ni kumi na sita, ambao waliuawa na "wakufunzi wa Urusi wa kampuni ya jeshi ya Wagner".

Wanamgambo wanaotajwa kama "mamluki" na wataalam wa Umoja wa Mataifa ambao pia walitajwa kuhusika na mauaji hayo na kundi la waasi la MKMKS la waziri wa zamani Jean-Serge Bokassa na muungano wa COD-2020 ambao unaleta pamoja viongozi wakuu wa upinzani wa kisiasa. Wapinzani wanalaani "mauaji mabaya" na wanadai kuundwa kwa "tume huru ya uchunguzi."

Wabunge saba kutoka mkoa wa Ouham wanasema katika barua ya wazi kwamba "wamehuzunishwa" na "mauaji ya raia na wafanyabiashara katika jimbo hilo" na kuitaka serikali "kutoa mwanga kuhusu tukio hilo".

Tume ya Umoja wa Mataifa, MINSUCA, ambayo imethibitisha kupatikana kwa angalau miili kumi na tatu, imetangaza kwamba uchunguzi unaendelea na "inaomba ushirikiano wa serikali".