CAMEROON

Cameroon: Wanajeshi sita waangamia katika shambulio la Boko Haram

Wanajeshi wa jeshi la Cameroon walipelekwa kwenye kituo cha Mabass, kwenye mlima karibu na mpaka na Nigeria, chini ya vijiji vinavyodhibitiwa na Boko Haram.
Wanajeshi wa jeshi la Cameroon walipelekwa kwenye kituo cha Mabass, kwenye mlima karibu na mpaka na Nigeria, chini ya vijiji vinavyodhibitiwa na Boko Haram. RFI/OR

Angalau wanajeshi sita wa Cameroon waliuawa Jumamosi katika shambulio la Boko Haram kaskazini kabisa mwa nchi hiyo, ambapo wanajihadi wameongeza mashambulizi, gavana wa mkoa huo amesema kwenye runinga ya serikali.

Matangazo ya kibiashara

Boko Haram walifanya shambulio kwenye kituo cha jeshi huko Sagme, karibu na mpaka na Nigeria, kaskazini kabisa mwa nchi hiyo Jumamosi asubuhi. Eneo ambalo Boko Haram imekuwa ikitekeleza mara kwa mara mashambulizi.

Idadi ya vifo ni angalau sita. Gavana wa mkoa wa kaskazini amewataka raia kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuwafichua wapiganaji na wanamgambo wa kundi la Boko Haram na waalifu wengine.