ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Wanafunzi elfu kadhaa wakwama katika mkoa wa Tigray

Kituo cha mabasi cha Mekele.
Kituo cha mabasi cha Mekele. RFI/Léa-Lisa Westerhoff

Hali katika jimbo la Tgray imeendelea kuzua wasiwasi mkubwa, wakati watu na wanafunzi kadhaa wamekwama katika jimbo hilo linalokabiliwa na mapigano kati ya waasi wa TPLF na vikosi vya Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

Wazazi wa wanafunzi hao wanaomba msaada wa kuwaondoa watoto wao katika jimbo laTigray.

Tangu vikosi vya waasi kutoka Tigray kudhibiti mji wa Mekele, mitandao ya mawasiliano imekatwa tena, na barabara nyingi katika mkoa huo zimefungwa. Wakati huo huo kumeripotiwa uhaba wa chakula.

Kwa jumla, zaidi ya watu milioni tano wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu, kulingana na Umoja wa Mataifa. Wazazi wanasema hawana taarifa kuhusu watoto wao wanaosomea katika mkoa huo kwa karibu mwezi mmoja. Wanafunzi katika vyuo vikuu vinne vya umma hawawezi tena kuwasiliana na familia zao.

Mamia kadhaa ya wazazi walikusanyika siku ya Ijumaa mbele ya ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Addis Ababa, wakiomba Umoja wa Mataifa kuingilia haraka ili kuwaokoa watoto wao waliokwama katika jimbo la Tigray.

Chuo kikuu chatoa wito kwa serikali kuchukua hatua

Mapema mwezi huu, Wizara ya Sayansi na Elimu ya Juu iliwatuliza nyoyo wazazi hao, ikisema kupitia Facebook kwamba wanaendelea na masomo kama kawaida.

Lakini siku ya Alhamisi, Chuo Kikuu cha Mekele kilitoa taarifa ya kutatanisha. Wakati chuo hicho kikuu kinafadhiliwa na serikali ya Ethiopia, kilibaini kwamba  hakijapokea fedha yoyote kwa mwaka huu. Na kinakosa pesa za kuwalisha wanafunzi. Na akaunti za benki zimezuiwa, hakuna ununuzi wa chakula unaowezekana. Chuo hiki kinasema kuwa hakitaweza kuchukua jukumu la kuwalisha wanafunzi kuanzia Julai 27.

Chuo kikuu kinatoa wito kwa mamlaka ya Ethiopia kupata suluhu y hali hiyo kabla ya tarehe hiyo. Ama kutuma pesa zinazohitajika au kutuma mabasi ili kuwhamisha wanafunzi kutoka jimbo la Tigray.