TUNISiA-SIASA

Rais Kaïs Saïed amfukuza kazi Waziri Mkuu na kusitisha shughuli ya Bunge

Kaïs Saïed, Rais wa Jamhuri ya Tunisia.
Kaïs Saïed, Rais wa Jamhuri ya Tunisia. Anis Mili/AFP

Rais wa Tunisia Kaïs Saïed ametangaza Jumapili jioni kwamba amesitisha kazi ya Bunge na kumuachisha kazi kiongozi wa serikali Hichem Mechichi, baada ya maandamano makubwa yaliyofanyika dhidi ya viongozi wa Tunisia.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imepelekea mamia ya maelfu ya Watunisia kumiminika mitaani Jumapili jioni, baadhi wakishangilia hatua hiyo, huku wengine wakitaka kujuwa kinachotokea.

Baada ya maandamano ya kisiasa kote nchini, rais aliwakutanisha viongozi wa kijeshi na polisi. Rais Kaïs Saïed alitangaza kwamba anamfuta kazi Hichem Mechichi, kiongoz wa serikali, na kwamba atateua mrithi wake ambaye atatangaza timu mpya ya mawaziri katika siku zijazo.

"Tunatangaza hatua nyingine za kuokoa Tunisia. Raia wa Tunisia lazima waendelee na mapinduzi yao katika njia halali inayowezekana na tutatumia sheria, ”alitangaza baada ya mkutano wa dharura katika ikulu ya Carthage na maafisa wa vikosi vya usalama. "Tunapitia wakati mgumu sana katika historia ya Tunisia," ameongeza rais Kaïs Saïed.

"Hii sio kusimamishwa kwa Katiba wala kukiuka katiba, tunafanya kazi kulingana na mfumo wa sheria", rais Kaïs Saïed amebaini akijitetea kuhusu Ibara ya 80 ya Katiba inachomruhusu kuchukua hatua za kipekee iwapo kutakuwa na hatari kwa nchi ya Tunisia. Lakini ibara hii hayajafahamika wazi juu ya hatua hizi, na hakuna kinachobainishwa juu ya kufutwa kazi kwa kiongozi wa serikali, wabunge kuvuliwa kinga, au kusitisha shughuli ya Bunge kwa mwezi mmoja, kama alivyotangaza rais Kaïs Saïed katika taarifa kwenye Facebook.

Chama cha Ennahdha chalaani "mapinduzi"

Kulingana na ibara hiyo, rais lazima pia awasilishe hatua yake kwa Mahakam ya kikatiba, ambayo haipo kwa sasa nchini Tunisia.