LIBYA-USALAMA

Mediterania: Wahamiaji wasiopungua 57 waangamia katika pwani ya Libya

Wahamiaji wanasubiri kuokolewa katika pwani Libya, Machi 20, 2017.
Wahamiaji wanasubiri kuokolewa katika pwani Libya, Machi 20, 2017. Abdullah ELGAMOUDI / AFP

Karibu wahamiaji 60 wamefariki duni katika pwani ya Libya wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania ili kuingia Ulaya, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM.

Matangazo ya kibiashara

Karibu wahamiaji 60, wakiwemo wanawake na watoto, wamifariki dinia baada ya boti lao kuzama Jumatatu wiki hii katika paniya Libya, mkasa mpya wa wahamiaji haramu katika Bahari ya Mediterania, liliripoti Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

"Wahamiaji wasiopungua 57 walikufa maji katika ajali ya boti katika iliyotokea kwenye mji wa Khoms Jumatatu hii," IOM ilisema. Jiji la Khoms linapatikana kilomita 120 kutoka mji mkuu Tripoli katika pwani ya magharibi ya Libya, nchi ya Afrika Kaskazini ambayo ilitumbukia katika machafuko tangu mwaka 2011.

"Manusura ambao walizungumza na wafanyakazi wetu walisema wanawake 20 na watoto wawili ni miongoni mwa waliopoteza maisha, "IOM imeongeza kwenye akaunti yake ya Twitter.

IOM haijatabainisha uraia wa wahamiaji hao, lakini picha zilizotolewa na shirika hilo zinaonyesha wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada wakitoa chakula na maji kwa manusura walioonekana wamechoka, wote wakionekana kutoka nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Libya ni sehemu muhimu ya kupitia kwa maelfu ya wahamiaji wanaotafuta kila mwaka kuingia Ulaya kupitia pwani za Italia, umbali wa kilomita 300 kutoka Libya. Idadi ya wahamiaji waliokufa baharini wakijaribu kuingia Ulaya imeongezeka zaidi ya mara mbili mwaka huu, IOM ilisema katikati ya mwezi Julai. Karibu watu 900 wamekufa maji  katika Bahari ya Mediterania mwaka huu.