TUNISIA-SIASA

Mgogoro wa kisiasa Tunisia: Waziri Mkuu kuachia madaraka

Gari la jeshi, mbele ya mlango wa Bunge la Tunisia, huko Tunis, Jumatatu Julai 26, 2021.
Gari la jeshi, mbele ya mlango wa Bunge la Tunisia, huko Tunis, Jumatatu Julai 26, 2021. © REUTERS - Zoubeir Souissi

Waziri Mkuu wa Tunisia Hichem Mechichi amesema yuko tayari kuachia ngazi na kukabidhi madaraka kwa Waziri Mkuu ajaye atakayeteuliwa na rais Kais Saied, siku moja baada ya kusitiishwa kwa shughuli za Bunge, uamuzi ambao ulizua sintofahamu katika nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro kwa miezi kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

"Niko tayari kukabidhi madaraka kwa waziri mkuu atakayeteuliwa hivi karibuni na rais wa Jamhuri," amesema Mechichi, katika taarifa yake ya kwanza tangu hatua ya Jumapili jioni. Chama tawala, cha Ennahdha, ambacho kinamuunga mkono Bwana Mechichi, kilisema kuwa maamuzi ya rais yalilenga kufanya mapinduzi ya serikali.

Hali inayojiri nchini Tunisia imeendelea kutia wasiwasi kwa mataifa ya kigeni. Ufaransa imesema inataka "kurudi, haraka iwezekanavyo, kwa shughulizi za kawaida za taasisi" na kuepusha vurugu zote, wakati Marekani, "inayotiwa wasiwasi na hali hiyo", imetaka "kulindwa kwa demokrasia" nchini humo.

Rais, pia alimfuta kazi Waziri wa Ulinzi Ibrahim Bartagi na msemaji wa serikali Hasna Ben Slimane, pia waziri wa Kazi na Kaimu Waziri wa Sheria, Jumatatu.